Habari Zote
MAAFISA kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Abeid Amani Karume cha Zanzibar (AAKIA), wamefurahishwa na namna ulinzi na
usalama wa abiria na mali zao unavyofanywa kwenye Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), imeelezwa.
Maafisa hao kutoka Idara mbalimbali walitoa kauli
hiyo jana katika ziara ya siku moja ya mafunzo JNIA, ambapo walitembelea maeneo
mbalimbali na kupata maelezo ya kina kutoka kwa maafisa husika.
Mkuu wa msafara wa maafisa hao, ambaye ni Mkuu wa
Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha AAKIA, Shaaban Kombo alisema JNIA inaulinzi
madhubuti kwa abiria na mizigo hukaguliwa kwa kutumia mitambo maalum kabla ya
kupanda ndege au kuingia ndani ya jengo kwa kazi mbalimbali, ambapo wameahidi
kufuata nyayo hizo ili kuzuia uhalifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.
Kombo alisema pamoja na kupata mambo mengi ya msingi
ya uendeshaji wa viwanja vya ndege, JNIA imekuwa darasa tosha, ambapo pia
katika upande wa utoaji wa vitambulisho wamejifunza namna utoaji wa
vitambulisho unavyofanyika, ukiwa ni tofauti na AAKIA ambao hutoa vitambulisho
vya kudumu mara baada ya taratibu kukakamilika, wakati JNIA hutoa vitambulisho
vya muda kwa muombaji ili aweze kuendelea na kazi, wakati akisubiri cha kudumu kikamilike
kutengenezwa.
“Tumefaidika na mambo mengi ukiangalia sisi kwetu
hii ya vitambulisho ni tofauti kabisa, ila kwetu kwa kipindi chote mteja
anasubiri kitambulisho cha kudumu anakuwa hawezi kuendelea na kazi zake eneo la
kiwanja hadi atakapopata cha kudumu, lakini hapa anakuwa na cha muda
kinachomfanya aendelee na shughuli zake huku cha kudumu kikiwa katika
matengenezo,” alisema Kombo.
Naye Mkuu wa kitengpo cha Ulinzi na Usalama cha
JNIA, Lugano Mwansasu alisema ziara ya maafisa wa AAKIA imewafariji na kuanza
ukurasa wa mahusiano katika ushirikiano, ambapo nao wamejifunza kulingana na
maelezo ya uendeshaji wa AAKIA.
Lugano alitoa wito kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), kuiga mfano huu wa kupeleka maafisa wake kwenye viwanja
mbalimbali vya nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza utendaji kwa lengo la
kuboresha huduma za viwanja kwa ujumla. TAA inasimamia viwanja 58 vilivyopo
chini ya serikali.
“Kila siku mambo ya uendeshaji yanabadilika, basi
tunaiomba mamlaka yetu itusaidie na sisi kwenda kutembelea viwanja vya wenzetu
tujifunze huko, zipo changamoto labda sisi hatujui zinatatuliwaje lakini kwa
ziara za mafunzo tunaweza kupata mbinu kutoka kwa wenzetu,” alisema Lugano.
Katika hatua nyingine, Meneja Uendeshaji wa JNIA, Vedastus Fabian alisema faida ya ziara ya mafunzo ni kujijengea uwezo na
mahusiano mazuri baina ya kiwanja kimoja na kingine.
Fabian alisema ziara hizo zinasaidia katika
kutatua matatizo yanayovikumba viwanja vya ndege, ambapo kwa sasa kumekuwa na
masuala ya ugaidi, uvushaji wa dawa za kulevia na nyara za serikali.
HUJAFA hujaumbika,
msemo huu wa lugha ya Kiswahili unawiana na hali ya kijana, Joseph Chacha,
aliyezaliwa akiwa mzima mwenye kutembea kwa kutumia miguu yake
miwili, lakini leo hii amejikuta akihitaji msaada wa kutumia baiskeli ya
walemavu kwa ajili kumsaidia katika matembezi yake.
Kijana Chacha
alizaliwa mwaka 1995 Bunda, mkoani Mara, ambapo mwaka 1998 alipata homa ya
kichocho na kumsababishia ulemavu wa kupooza viungo vyote mpaka hivi sasa.
Anasimulia kuwa
umasikini wa kipato unao ikabili familia yake unamchango mkubwa katika ulemavu
alionao, kwani kulikua na uwezekano mkubwa wa kupona nakumaliza tatizo hilo
kama angepata matibabu stahiki.
“Magonjwa mengi
nchi za Afrika yanasabisha kukwamisha ndoto za watu wengi hususan sisi masikini. Tatizo
langu lilikuwa gumu na kuniathiri siku hadi siku kutokana na umasikini,
kama familia yangu ingekuwa na pesa basi ningepata matibabu
yanayostahili,” anasema Chacha.
HARAKATI ZA
MATIBABU
Katika mahojiano
na mwanasafu wa kurasa hii (Tuishivyo), kijana huyo anaeleza baada ya kutokea
kwa tukio hilo wazazi wake walimpeleka Hospitali ya Wilaya ya Bunda ambako
alipata matibabu, lakini hayakumsaidia, ndipo wakaamua kwenda kwa mganga wa
tiba za asili kwa ajili ya kupata matibabu lakini nako hakupata nafuu
badala yake wakaamua kurudi nyumbani kutokana na kukosa fedha kwa ajili ya
kuendelea kupata matibabu.
“Nilipelekwa
hospitali nikapata matibabu madaktari wakasema nina homa ya kichocho nikapata
nafuu lakini baadae homa iliendelea ndipo wazazi wangu wakaamua kunipeleka
kwenye tiba za asili homa ikaisha bali viungo vyangu vikaanza kushindwa kufanya
kazi mpaka hivi sasa.”
HARAKATI ZA
MAISHA
Pamoja na hali
yake hiyo ya ulemavu, umasikini wa familia yake, kushindwa kumudu matibabu na
mahitaji ya kila siku ya nyumbani kutokana kuishiwa kabisa pesa ya kupata
mahitaji, alimuomba mama yake ampeleke katika shule za wanafunzi wenye ulemevu
ili ajue kusoma na kuandika kwa ajili ya kuendeleza ndoto zake.
Mwaka 2007
alipelekwa Shule ya Msingi Nyansror iliyopo Bunda ambako alijifunza kusoma na kuandika lakini mwaka 2012 aliacha
kusoma akiwa darasa la tano kutokana na wazazi kushindwa kumudu gharama
za mahitaji ya shule pamoja na kumwongoza kutokana na uzee.
“Sikupenda
kuacha shule kwani nilikuwa na ndoto za kuendelea na shule ndio maana
nilichelewa kuanza lakini nikaona bora nisome ili niweze kufanikisha malengo
yangu, sikukata tamaa kwasababu ya hali yangu ila ilinilazimu kuacha
masomo baada ya mama yangu ambae ndio msaidizi wa maisha yangu kufariki, hapo
ndipo ugumu wa maisha ulipoanza kutokana baba yangu alikuwa mzee pia alikuwa
mlemavu wa mguu mmoja,” anasema.
CHANGA MOTO ZA MAISHA
Kijana Chacha anaeleza
katika maisha yake amepitia changamoto nyingi sana, ikiwamo baada ya kufiwa na
mama yake akanza kuombaomba misaada mbalimbali ikiwamo kanisani ili apate fedha
kwa ajili ya kusukuma maisha yao. Anasema alipoona hali inazidi kuwa ngumu
aliamua kwenda kutafuta maisha jijini Dar es Salam.
Anasema
alifika Dar es Salaam mwaka 2012 na kuanza kuombaomba na kwamba alipata changamoto mbalimbali ikiwamo kukoswa
kugongwa na magari alipo kuwa barabarani, huku akilala na kuomba misaada stendi
ya mabasi ya mikoani ya Ubungo.
Anasimulia kuwa
alipatwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) hivi karibuni kutokana na kulala nje
kila siku.
WITO
Chacha anatoa
rai kwa wanajamii wote wanaoguswa na changamoto zinazowakabili walemavu kumsaidia
kwa kumchangia fedha ili aweze kupanga
na kuishi katika chumba chake na kupata mahitaji muhimu ya kila siku.
Aidha, anaiomba
serikali na wadau mbalimbali kumuonea huruma na kumnunulia bajaji pamoja na kumpatia
mtaji wa kufanyia biashara ili aweze kufanya biashara na kuendesha maisha yake.
“Nawaombe wadau
mbalimbali na serikali kunisaidia kupata mtaji ili nifanye biashara
nijimudu kimaisha, Watanzania wenzangu mimi sikupenda hii hali naumia
kulala nje kila siku nalazimika kuishi barabarani sina pa kukaa, nakula kwa
kutegemea wasamaria wema ambao wanafanyakazi maeneo hayo, pia namshukuru Mbunge
wa Ubungo, Saidi kubenea, alinipatia baiskeli hii kipindi cha kampeni ingawa
hivi sasa imeisha matairi yamepasuka kama unanyo yaona,” alisema Chacha kwa
huzuni kubwa.
TAHARIRI:
HAKUNA
mashaka kwamba sasa tatizo la mafuriko sio kadhia kwa `watu wa mabondeni’ au wanaoishi karibu na mkondo wa
maji pekee.
Hata
hivyo, nguvu kubwa imekuwa ikiwekwa katika
kuwahamisha watu wanaoishi kwenye maeneo hayo bila kutafuta na kuthibiti
chanzo cha mafuriko hayo.
Mathalani,
katika jiji la Dar es Salaam, tumekuwa
tukishuhudia wakazi wa Bonde la Mto Msimbazi, Mkwajuni, Jangwani na kwingineko jijini humo wakihamishwa, baadhi nyumba zao
kuvunjwa.
Oktoba
26 mwaka huu, ilinyesha mvua kubwa nchini
na kusababisha madhara makubwa hasa jijini Dar es Salaam, kwa mafuriko ya mvua hizo kuua
watu kadhaa, kuharibu mali zenye thamani
kubwa.
Kila
mtu atakuwa shahidi kupitia vyombo vya habari kuwapo kwa malalamiko ya athari
za mafuriko hayo kila kona ya jiji na
maeneo mengine nchini.
Kama
tulivyosema nguvu kubwa huelekezwa kwenye kuhamisha watu, hakuna juhudi za kukabiliana na chanzo cha mafuriko.
Ni kuokoa au kuhamisha tu.
Sisi
tunaikumbusha serikali wajibu wake wa kuwalinda wananchi wake dhidi ya majanga
kwa kutambua kwamba chanzo cha mafuriko ni ongezeko la maendeleo ya watu
(Human
Development Expansion) tunayoyataka!
Yapo
maendeleo ya ongezeko la nyumba, shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, biashara na viwanda ambazo
watalaamu wanasema vimekuwa chanzo cha ongezeko la mafuriko na kina cha maji ya
bahari.
Kwa
hiyo matatizo kama mmomonyoko wa udongo unaotokana na maji mengi yasiyovunwa
kwenye nyumba, kukosekana kwa vizuia kasi ya maji kama vile miti kutokana na mabadiliko
ya tabia nchi hujitokeza.
Matokeo
yake ni kupanuka kwa makorongo, mito, bahari na maziwa kila uchao na kupatikana kwa mabonde.
Bila
kutambua wajibu wake katika kukabiliana na hali hiyo, serikali hukimbilia
kuwaondoa watu kwa kigezo cha kisheria kwa kuwaita wavamizi wa mita 60 za mito, bahari na maziwa tena wengine sheria ya mazingira ya (EMA) ya
mwaka 2004 iliwakuta.
Sisi
tunaona kwamba kuna kila sababu ya serikali kutafuta chanzo cha mafuriko na kukithibiti.
Hii ni pamoja na kujenga kingo za mito, bahari na maziwa ili kutopanuka na
kufuata makazi ya watu.
Huu
ni wajibu kulingana na mikataba ya kimataifa ambayo serikali yetu ilisaini na
ni haki ya wananchi wa nchi husika.
Tunapokimbilia
kuwahamisha watu wakati mabonde yalitokea kwa kutojengwa kingo, ni wazi kwamba
hata wale ambao leo wako nje mita 60 kesho watakosa uhalali wa kuishi humo
kutokana na mmomonyoko unaoendelea kuwafuata. Tutawahamisha wangapi? mwisho
tutahamisha mtaa mzima!
Pia
tunaishauri serikali kuimarisha miundombinu kwa kujenga au kufufua mitaro
kutokana na ukosefu wa mitaro kusababisha kuzagaa kwa maji na kuwa chanzo kwa watu wengine ambao sio wa mabondeni nao
kuingia katika kadhia hiyo.
Sisi
tunaamini kwamba hayo yakitiliwa mkazo tutapunguza au kumaliza tatizo la mara
kwa mara la mafuriko. Haina maana kwamba waliojenga baada ya sheria waachwe.
Msisitizo wetu ni jamii kutii sheria sambamba na kuthibiti chanzo cha tatizo
kama haki ya jamii.
Kuwahamisha
watu sio suluhisho na kukomesha tatizo. Ni sawa na kugawa vyandarua badala ya
kuua mazalia ya mbu!
KILA
mtu ana ndoto ya kufikia lengo fulani katika maisha yake. Na hapo ndipo hutimia neno
la kitaalamu lisemalo: ‘Maandalizi ya leo ni mafanikio ya kesho’ au maisha ni
mchakato, hatua’.
Kijana Joas Yunus kwa muda mrefu amekuwa na ndoto ya kuwa
mwandishi wa wa vitabu kwa ajili ya kuielimisha jamii kupitia fasihi andishi
iliyoianza tangu akiwa mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi
Nzovwe iliyoko wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.
Anasema tangu akiwa darasa
la nne alipenda kufundisha japo hakujua atafundisha kwa njia gani, hivyo aliamua
kujitolea kuwafundisha wanafunzi wenzake walio madarasa ya chini yake, baadaye kuanzisha kituo cha mafunzo kwa watoto wadogo ambacho
aliendelea nacho hata baada ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2003.
Alisema ili kutopoteza ndoto yake, aliendelea
kujitolea kuwafundisha hata baada ya kuendelea na masomo ya sekondali ingawa
alipatwa na changamoto nyingi kwa kuwa haikuwa rahisi kuwafundisha aliokuwa
anasoma nao darasa moja na wakamkubali wote.
Hata hivyo, pamoja na changamoto
alizopata hakukata tama na alipohitimu sekondari aliendelea kufundisha masomo
ya jioni katika kituo alichokianzisha nyumbani kwao kabla ya kupata nafasi ya
kujiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Pugu mwaka 2008.
Baadaye alipogundua kwamba kufundisha kuna tija kwa jamii, akaamua
kuwashirikisha baadhi ya wenzake ili kuandika vitabu.
Aligundua kwamba ili vitabu viwe bora, kusomwa zaidi na kuongeza soko
anatakiwa atafute watu wenye uwezo wa kusanifu hasa upande wa marafiki zake.
Ubunifu wake huo ulimsaidia kuongeza kipato na kufanikiwa kupata
mtaji wa kuzalisha matoleo mengine zaidi huku akiendelea na masomo yake pamoja
na kuendeleza kituo chake alichokuwa amekianzisha mkoani Songwe hadi alipoanza elimu
ya juu.
Anasema aliendelea na kituo chake hicho na kufanikiwa kugawa mtaji kwa kuanzisha kituo
kingine cha elimu kwa
vijana na watu wazima pasipo gharama zozote kwa nia ya kuisaidia jamii yake.
Baada ya kurudi kijijini kwao alifanya
ibada zake katika kanisa la FPCT na kuchaguliwa kuwa katibu wa vijana kanisani
baada ya kumpenda kutokana na uandaaji, uandishi na mpangilio mzuri wa taarifa
za vikao vya kanisa.
Kazi yake ya kuisaidia jamii ikamfanya apate umaarufu zaidi na kuchaguliwa
kuwa katibu wa vijana katika kanisa la FPCT alilokuwa akifanya ibada.
Yunus alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2010 na
kupata Shahada ya Sayansi ya Kompyuta na
baadae elimu mbalimbali ya ujasiriamali.
“Pia nilifanikiwa kusoma shahada ya elimu sayansi ya kompyuta na
baadaye ujasiriamali. Niliweza kusoma na kufanya kazi zangu
kuhakikisha tu kwamba vitabu vipo katika usahihi,” alisema.
Anasema akiwa katibu alipata wazo jingine
katika kutoa huduma kwa vijana wengine nje ya kanisa hivyo akamua kusajili kitabu
chake alichokiita ‘Kijana jitambue’
kilichokuwa na maudhui ya kutoa elimu mbalimbali kwa rika ili waweze
kujitathmini na kujitambua hasa katika kuziona fursa mbalimbali na
kuzichangamkia.
Mwaka 2015 aliandika kitabu kingine
alicho kiita ‘Inuka’ kwa maana ya inuka katika dimbwi la umasikini na kujifunza
ufundi wa magari mtaani.
Anasema alikuwa hana uhakika wa kupata
kazi, jambo lililomsukuma kubuni njia ya kupata kazi. Anasema aliamua kupanga
makopo matupu ya oili pembeni mwa barabara ya zamani ya Bagamoyo ili kuwavuta
watu walioharibikiwa na magari.
“Ndipo
siku moja, raia mmoja wa kigeni akaona yake makopo na kushuka kutoka ndani ya
gari. Kisha nilimsogelea na kugundua kuwa gari yake ilikuwa na hitilafu iliyosababisha
isiwake, niliitengeza na kulipwa pesa ambayo kwangu ilikuwa mtaji,”anasema.
Anasema changamoto zilizopo katika kazi
yake ya uandishi ni pamoja na kutokuwa na watu wanaoweza kumuwezesha pamoja na
kukosa vitendea kazi kama vile kompyuta
Yunus kwa sasa meamua kujiajiri kupitia
fani yake ya uandishi wa vitabu na kuwashauri waandishi wengine kuandika kwa
ajili ya jamii na Tanzania ya viwanda iweze kuendelea mbele pamoja na kuanzisha
vituo vingi vya kutoa mafunzo kwa vijana
katika kila wilaya.
JAMII imeshauriwa kujiunga kwenye vikundi ili
kuunganishwa kwenye mfumo wa teknolojia ya usafishaji wa maji taka kwa ajili ya matumizi mengine ili
mfumo huo uwasaidie kutumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali zenye tija badala
ya kuyateketeza baada ya matumizi.
Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya kuhamasisha matumizi endelevu ya maji taka
(OSWAMS), Juma Mohamed Nasoro katika ziara ya maofisa mbalimbali wa
serikali walipokuwa wakitembelea mradi
huo unaotekelezwa katika nyumba za maofisa wa jeshi la polisi, mikocheni jijini Dar es Salaam.
Alisema tekonolojia ya usafishaji wa maji taka ni
muhimu wakati huu taifa likihitaji watu wake kuwajibika ipasavyo kwa kuanzisha
miradi ya uzalishaji mali kufikia uchumi
wa kati kwa njia ya viwanda.
Kwa bahati mbaya, sehemu kubwa ya watu hawajatambua
fursa zilizopo katika matumizi ya teknolojia hiyo na kusababisha maji taka yanayozalishwa
kuteketezwa wakati yangetumika kwa ajili
ya shughuli za kilimo, ufugaji wa samaki, ujenzi na bustani.
“Maji machafu ni fursa sio tatizo. Kwa hali ilivyo
sasa kila hitaji la maji lazima yatumike maji ya Dawasco. Tunataka maji taka
yasafishwe na yatumike kwa shughuli za kuongeza kipato sio kutegemea maji ya
Ruvu chini na Juu. Ili kufikia malengo haya ni lazima elimu ipelekwe kwa
wananchi ya umuhimu wa teknolojia hizi ambayo pia huzuia magonjwa hasa ya
mlipuko,”alisema.
Akifafanua kuhusu mfumo huo wa kutibu maji taka,
Nasoro alisema kabla ya maji hayo kutumika hupitia hatua kadhaa kuanzia
utengenezaji wa chemba ambayo ni ya kwanza ya matibabu ya maji hayo.
Kisha maji taka hupitishwa kwenye mfumo wa pili wa tiba unaojulikana kitaalamu kama
anaerobic (ABR) na U-Flow Anaerobic (UAF ) ambapo wadudu hula takataka kabla ya
kufikia kiwango cha juu cha udhibiti, alisema.
“Maji yanayotibiwa kwa njia hizo yanakuwa yametibika
kwa asilimia 85 na kiasi kingine huenda aridhini. Kwa hali hii sio rahisi
kusababisha magonjwa, ni salama kwa matumizi kwani yamesafishwa kitaalamu.
Yanafaa sana kwa kilimo na ufugaji kwani yana mbolea, nitrogen na
phosphorus,”alisema.
Alisema kampuni yake imefanikisha teknolojia hiyo
katika taasisi za umma na shule binafsi ya Libermann ya pia ya jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya maofisa waliotembelea mradi huo kutoka
wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto, Jiji la Dar es
Salaam na Manispaa za Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo waliridhishwa na
utekelezwaji wa mpango huo na kusema hatua inayotakiwa ni jamii kuhamasishwa
kujiunga baada ya kuutathimini na kuingizwa kwenye mipango ya ya serikali.
Afisa afya wa Manispaa ya Ubungo Wilson Msangi
alisema teknolojia hiyo ni hupunguza gharama ya ukusanyaji wa maji taka,
huchukua nafasi ndogo na kushauri Halmashauri kuihamasisha kwenye maeneo kama
shule na hospitali kutokana na maeneo hayo kuzalisha kiasi kingi cha maji taka.
· Yamo
kisukari, saratani, presha, hamu ya tendo
MMEA wa bamia uzaao matuda yanayoliwa, ni zao
linalostawi karibu maeneo yote hapa nchini, ingawa hustawi na hupedwa zaidi na
watu wa ukanda wa Pwani. Huliwa kama mboga kwa matunda hayo kupikwa
yakichanganywa na aina nyingine ya mboga kama vile nyama.
Watu wa ukanda wa Pwani hutumia bamia kwa
kuikatakata vipande vidogo na kuchanganya vipande hivyo na majani ya maboga, magadi kisha kupika pamoja na
kupata mboga iitwayo mlenda au hombwe kwa watu wa pwani ya mkoa wa Tanga.
Kwa bahati mbaya sana walaji wengi hawajui umuhimu
wake kifya kama anavyobainisha Mtaalamu na Mkufunzi wa Chuo cha Tiba na Uuguzi
( IMTU) cha jijini Dar es salaam, Dk. Daniel Elifariji Mtango.
Mtaalamu huyo wa kitengo cha Afya na Jamii Chuoni
hapo, anasema tunda la bamia lina vitamini A na B ambavyo huimarisha macho kutokana
na virutubisho hivyo kusheheni kiasi
kingi cha protini ukilinganisha na lishe nyingine inayotokana na mimea.
Kama hiyo haitoshi, viini lishe vilivyomo husaidia kuwaokoa
watoto wenye tatizo la utapiamlo, isulini kufanya kazi
hivyo kuwaondoa watu katika hatari ya ugonjwa wa kisukari kwa kuuweka sawa mfumo wa sukari mwilini.
Zinapoliwa kwa usahihi, huongeza kinga za mwili kwa
watoto na watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka na kuwa kwenye hatari ya
kuambukizwa Virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine yanayosababishwa na kushuka
kwa kinga ya mwili, anasema.
Akifafanua zaidi, Dk. Mtango anasema, maji ya bamia husaidia
kuzuia magonjwa ya moyo kwa kuifanya mishipa ya damu kufanya kazi vizuri
kutokana na maji yake kuwa uwezo wa kuondoa lehemu kwenye kuta za mishipa ya
damu.
“Lehemu zisipoondolewa kwenye mishipa hiyo
husababisha msukumo wa damu kwenda vibaya na kuwa chanzo cha maradhi ya shinikizo
la damu. Kwa hiyo tunaona ni kwa jinsi gani ambavyo mmea huu ulivyo muhimu
katika lishe na kudhibiti magonjwa ambayo wakati mwingine hayawezi kutibiwa
hapa nchini. Hivyo bamia inaweza kupunguza idadi ya watu kwenda India kutibiwa
maradhi ya moyo,”anasema,
Faida zingine za ulaji wa bamia ni kuzuia tatizo la watoto kupasuka uti wa
mgongo au mgongo waz, kumsaidia mama mjawazito pamoja na mtoto tumboni kuwa na afya
na baada ya kujifungua.
Hutibu tatizo la kuchoka bila sababu, zaidi kwa watu ambao wana msongo wa mawazo ambao
mtaalamu anashauri kundi hilo kula kwa wingi bamia kwani huleta matokeo ya
haraka na kufanya afya zao kuimarika zaidi na kuwafanya wawe na amani, furaha muda wote.
Faida nyingine, hutibu vidonda vya tumbo na
kuthibiti bakteria wasababishao matatizo
hayo na kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo, huongeza kiwango cha
uzalishaji wa damu kwa wingi mwilini.
Huimarisha nywele na kuzifanya ziwe na muonekano
mzuri pamoja na kufanya utumbo mpana kubaki katika ulaini wa asili yake na kukinga mtumiaji dhidi ya saratani ya utumbo mpana (large intestine).
Pia hufanya mfumo wa usagaji wa chakula kuwa mzuri
na hivyo kupunguza maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa kutokana na majimaji
ya bamia hulainisha choo kama ilivyo papai na ndizi mbivu. Pia huongeza hamu ya
tendo la ndoa.
MATUMIZI:
·
Mlaji anaweza kupika bamia kama mboga kisha
kuchanganya na chakula kingine na kula kama mlo. Vyakula hivyo vinaweza kuwa, uji,
mchuzi, na vingine.
·
Matumizi mengine ni mtumiaji anatakiwa
kukatakata bamia vipande vidogovidogo baada ya kuoshwa kwa maji safi na salama.
Loweka kwenye maji kwa dakika kadhaa vipande hivyo kulingana na uwingi wa
vipande vyenyewe ili kupata juisi.
·
Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha juisi
ya bamia sawa na gramu 100. Au unaweza kula vipande hivyo vibichi vilivyojazwa
kwenye kikombe cha ujazo huo .
·
Inashauriwa kuwa watoto wadogo wapatiwe zikiwa zimepikwa. Fanya hatua hizo tatu kwa mfululizo na matokeo
yake hujitokeza kuanzia juma la tatu au kabla.
Anatoa ushauri kwa wakulima kulima zao hilo kwa wingi
kutokana na faida hizo za kiafya na kukifanya kilimo chao kuwa na tija.
Ni zao
linalokomaa kwa muda mfupi na hukabiliana na hali zote za hewa. Pia jamii kula
kwa wingi bamia ili kupunguza matatizo ya kiafya ambayo baadhi yake ameyaanisha katika makala
haya.
WANAFUNZI
wawili wa shule ya msingi Sarawe iliyoko katika tarafa ya Chamriho halmashauri
ya wilaya ya Bunda mkoani Mara, wamekufa na wengine sita kujeruhiwa katika
ajali mbaya ya kuangukiwa ukuta wa chumba cha darasa wakati wakipembua mahindi
kwa ajili ya chakula chao shuleni hapo.
Tukio hilo limetokea juzi majira saa kumi
jioni wakati wa saa ya mapumziko katika eneo la shule hiyo.
Wanafunzi waliokufa katika tukio hilo ni
pamoja na Anastazia Wazilana (8) aliyekufa papo hapo na Amosi Stima Igala (8)
aliyekufa wakati akikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza
kwa ajili ya matibabu zaidi, ambapo wote walikuwa wanasoma darasa la pili
shuleni hapo.
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Bunda
Dk. Nuru Yunge amethibitisha vifo hivyo na kwamba majeruhi walipelekwa kituo
cha afya Ikizu na wengine wamehamishiwa katika hospitali ya DDH Bunda.
“Pale kituo cha afya Ikizu tulipokea majeruhi
saba, na wengine wawili tukawahamishia katika hospitali ya DDH Bunda, kutokana
na hali zao kuwa mbaya, lakini kwa taarifa niliyopata majeruhi mmoja amekufa
wakati akipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando” alisema.
Afisa tarafa ya Chamriho Boniphace Maiga,
aliwataja wanafunzi waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Happynes Mussa (13) wa
darasa la tano, Wambura Nyamrosha (12) wa darasa la nne, Sara Wazilana (14) wa
darasa la sita, Emmanuel Mkiriti (8) wa darasa la pili, Mugaya Galinde (8) wa
darasa la pili na Pili Juma Matwiga (7) wa darasa la kwanza.
Maiga alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
ukuta wa darasa hilo kuwa na ufa wa siku nyingi, ambapo uliporomoka na
kuwaangukia wakati wakianda mahindi kwa ajili ya chakula cha wanafunzi shuleni
hapo, kinachotolewa na shirika la PCI.
“Wakati wa mapumziko wanafunzi hao walikuwa
nje ya dasrasa hilo wakipembua mahindi ya PCI na ghafla ukuta huo ulidondoka na
ulikuwa na naufa mkubwa siku ninyingi. Mwanafunzi mmoja alifia hapo hapo na
mwengine amekufa wakati akikimbizwa Bugano baada ya kuwapatiua rufa.
Baadhi ya mashuhuda akiwemo katibu wa huduma
za jamii katika serikali ya kijiji cha Sarawe, Richard Karangi, walilielezea
tukio hilo kuwa ni la kusikitisha, ambapo muuguzi mmoja katika hospitali ya DDH
Bunda, alizungumzia hali ya majeruhi mmoja aliyempokea kwamba inaendelea
vizuri.
Kamanda wa polisi mkoani Mara kamishina
msaidizi wa polis, Jafari Mohamed hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini
polisi wilayani hapa wamethimitisha kuwepo kwa tukio hilo.
Wakati huo huo, baadhi ya wananchi
waliozungumza na waandishi wa habari walisema kuwa ipo haja ya wakaguzi wa shule
kukagua majengo ambayo hayana ubora na kuagiza yasitumiwe na wanafunzi ili
kuepusha majanga kama hayo ambayo siyo
ya lazima yasitoke tena.
BOGA ni moja kati ya matunda yenye faida mbalimbali katika mwili
wa binadamu. Hupatikana karibu mikoa yote ya Tanzania, na idadi kubwa ya watu
wengi kulima boga kwa matumizi ya nyumbani kama chakula.
Wengi pia hawajui faida za tunda zaidi ya kulitumia kama chakula,
lakini ukweli ni kwamba matumizi yake ni zaidi ya chakula.
Boga huweza kusindikwa au kusagwa na kupatikana kimiminika (juisi)
muhimu kwa afya ya binadamu kwani hutibu magonjwa mbalimbali.
Dk. Othman Shemu ni mtaalamu wa miti na mimea dawa na Mkurugenzi mtendaji
wa kliniki ya tiba asili cha
Paseko yenye makao yake Tabata relini Jijini
Dar es Salaam, anasema juisi ya boga pia
huimarisha na kuongeza nguvu za kiume.
Huwafanya
wanaume kumudu tendo la ndoa hasa wale ambao huishia mshindo au pigo moja au
kushindwa kumfikisha kileleni mwanamke na wakati mwingine kukosa hamu ya tendo
la ndoa Anasema tunda la boga lina protini na virutubisho mbalimbali vyenye
uwezo wa kutibu magonjwa ikiwamo kutengeneza mbegu za kiume kwa wingi kama
ilivyo baadhi ya vyakula vya protini.
Baadhi
ya magonjwa hayo ni tezi dume, kusafisha figo, tatizo la kutapika mfululizo
hasa kwa mama mjamzito, huondoa tatizo ya gesi tumboni na msongo wa mawazo.
“Ukitunia
juisi hii huruhusu ubongo kuingiza hewa safi kwa wingi (oxgen) na kutoa hewa
chafu hali inayofanya ubongo kuwa mwepesi na kutunza kumbukumbu za kutosha, “
anasema Dk Shemu.
Pia
huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni na kuondoa vijidudu
visivyotakiwa tumboni, pamoja na kusaidia kurekebisha mfumo wa msukumo wa damu
kwa watu wenye matatizo ya presha.
Huweza
kutumiwa na rika za watu wote ingawa ni muhimu zaidi kutumiwa na watoto kwani
huwakinga na magonjwa na kuwasaidia kujenga uwezo wa kufikiri na kutunza
kumbukumbu (akili) jambo ambalo linaweza kuongeza ustawi wa masomo darasani.
UANDAAJI:
Shemu
ambaye pia ni katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Waganga (SHIVYATIATA)
anasema zipo njia mbalimbali za uandaaji wa ambapo mhussika anasema kumenya
maganda ya juu yasiyotakiwa kisha maandalizi kuanzia nyama (sehemu ya njano),
moyo na mbegu.
Chukua
nyama, kata vipande vidovidogo baada ya kusafishwa kwa maji safi na salama.
Jaza vipande hivyo kwenye mashine maarufu kama (Brenda) kwa ajili ya kusaga au
kusindika.
Unaweza
wakati wa kusindika unaweza kuchanganya vipande hivyo na ndizi, maji safi
kidogo ili kurahisisha usindikaji kutokana na ndizi na vipande vya boga kuwa
katika hali kavu.
Inashauriwa
kuwa juisi iliyosindikwa katika mchanganyiko huo ina ongezeko kubwa la
virutubisho kama vile kalishiamu husaidia watu wenye upungufu au ukosefu wa
kinga mwilini (UKIMWI) kuongeza kinga ya mwili.
“Pia
majaribio yetu yameonyesha kwamba juisi hii ikichanganywa na juisi ya maua
yajulikanayo kama rosemary maarufu kama rosella inakuwa na uwezo zaidi katika
tiba kutokana na virutubisho vingine kama kalishiam na magnesiamu vilivyomo
kwenye rosella,”alisema.
Zipo
aina mbalimbali za uandaji wa juisi ya boga kwa mtu mwenye tatizo la nguvu za
kiume hutakiwa, kuchukua boga na kulikata vipande vidogo vidogo na kusaga bila
vipande hivyo kuwa mbegu zake.
Anachotakiwa
mhusika kufanya ni kuzipaa mbegu za boga ili kuzitenganisha na nyama kisha
kuzianika sehemu yenye kivuli hadi zitakaponyauka, saga kwa ajili ya kupata
unga.
Inashauriwa
kusaga unga huo wakati wa matumizi tu kwani unga wake ukihifadhiwa muda mrefu
unaweza kusababisha mlundikano wa fangasi ambao ni hatari kiafya, alisema Dk.
Shemu.
MATUMIZI:
Unaweza
kunywa juisi ya boga iliyosindikwa na kuchanganywa na pensheni ili kuongeza
ladha (test) na sukari kidogo kadri unavyoweza kwasababu matumizi yake mengi
hayadhuru.
Kuhusu
unga wa mbegu za boga, mtumiaji mwenye matatizo hayo anatakiwa kuchukua unga
kwenye kijiko kimoja cha chai kisha kuchanganya kwenye glasi ya maji na kunywa.
“Kunywa
mara tatu kwa siku. Mwneye tatizo kubwa anapaswa kunywa katika muda wa siku 21
mfululizo. Kwa mwenye tatizo la msongo wa mawazo anaweza pia kunywa juisi ya
mchanganyiko wa ndizi mbivu na boga kwa kuchanganya na unga wa mbegu
hizo”alisema.
TANZANIA imezidi kupata neema kutoka Jumuiya ya Kimataifa ambapo Novemba 2, 2017, Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 50, takriban Shilingi bilioni 130 kwa ajili ya kufadhili Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Mkataba wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Neven Mimica.
Msaada huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya nishati ya umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao wa usambazaji umeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu wake.
“Umoja wa ulaya ni wadau wetu muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu na mikubwa wanayotupatia, na kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema James
Alisema kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo bila masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya viwanda itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Doto James alisema kuwa tangu Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini REA uanze miaka 9 iliyopita, idadi ya vijiji vilivyounganishiwa umeme imeongezeka kutoka vijiji 400 mwaka 2008 hadi kufikia vijiji 4395 hivi sasa.
Alisema kuwa ni matarajio ya Serikali kwamba ifikapo mwaka 2020, vijiji vyote 12,000 hapa nchini vitakuwa vimeunganishwa na nishati hiyo hivyo kuchochea shughuli za uzalishaji viwandani na kiuchumi kwa wananchi, vitaimarika.
Kwa upande wake, Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Neven Mimica, amesema kuwa msaada huo wa Euro milioni 50 wanaoutoa ni sehemu ya msaada wa Euro milioni 207 ambazo wanachama wengine wa Umoja huo, ikiwemo Sweden, Uingereza, Norway na Benki ya Dunia, watatoa kufanikisha mradi huo wa usambazaji umeme vijijini kupitia REA.
“Nguvu hizi za pamoja zitaviwezesha takriban vijiji 3,600 vilivyoko maeneo mbalimbali ya nchi ambapo watu zaidi ya milioni 1 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo” Alisema
Alisema hatua hiyo itachangia kuimarika kwa ubora wa maisha ya wananchi wa Tanzania, kuimarika kwa sekta za afya, elimu na kuleta faida za kijamii na kiuchumi zinazoonekana kwao moja kwa moja hususan wanawake na watoto.
Misaada ya Umoja wa Ulaya kwa Tanzania imejikita katika Nyanja tatu za Utawala bora, Umeme na Kilimo endelevu ambapo Umoja huo kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (EDF) umetenga kiasi cha Euro milioni 626 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014-2020
Mkataba wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Neven Mimica.
Msaada huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya nishati ya umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao wa usambazaji umeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu wake.
“Umoja wa ulaya ni wadau wetu muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu na mikubwa wanayotupatia, na kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema James
Alisema kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo bila masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya viwanda itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Doto James alisema kuwa tangu Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini REA uanze miaka 9 iliyopita, idadi ya vijiji vilivyounganishiwa umeme imeongezeka kutoka vijiji 400 mwaka 2008 hadi kufikia vijiji 4395 hivi sasa.
Alisema kuwa ni matarajio ya Serikali kwamba ifikapo mwaka 2020, vijiji vyote 12,000 hapa nchini vitakuwa vimeunganishwa na nishati hiyo hivyo kuchochea shughuli za uzalishaji viwandani na kiuchumi kwa wananchi, vitaimarika.
Kwa upande wake, Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Neven Mimica, amesema kuwa msaada huo wa Euro milioni 50 wanaoutoa ni sehemu ya msaada wa Euro milioni 207 ambazo wanachama wengine wa Umoja huo, ikiwemo Sweden, Uingereza, Norway na Benki ya Dunia, watatoa kufanikisha mradi huo wa usambazaji umeme vijijini kupitia REA.
“Nguvu hizi za pamoja zitaviwezesha takriban vijiji 3,600 vilivyoko maeneo mbalimbali ya nchi ambapo watu zaidi ya milioni 1 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo” Alisema
Alisema hatua hiyo itachangia kuimarika kwa ubora wa maisha ya wananchi wa Tanzania, kuimarika kwa sekta za afya, elimu na kuleta faida za kijamii na kiuchumi zinazoonekana kwao moja kwa moja hususan wanawake na watoto.
Misaada ya Umoja wa Ulaya kwa Tanzania imejikita katika Nyanja tatu za Utawala bora, Umeme na Kilimo endelevu ambapo Umoja huo kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (EDF) umetenga kiasi cha Euro milioni 626 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014-2020
NAIBU Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (Mb),
amewapongeza Wakala wa barabara nchini (TANROADS), kwa mikakati wanayotumia kudhibiti
vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini.
Akifungua
Mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi la TANROADS mjini Kigoma, Kwandikwa,
amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watendaji wake wote wanakuwa waadilifu
ili rasilimali chache zitumike kwa manufaa ya wote.
“Hakikisheni
kila mtakaye mkamata kwa vitedo vya rushwa hatua za kisheria anachukuliwa
ikiwemo na kufukuzwa kazi ili kuonyesha kuwa jambo la rushwa tunalichukia na hatulipendi
katika Serikali”, alisema.
Naye Mtendaji
Mkuu Wa Wakala huo Eng. Patrick Mfugale, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka
mmoja watumishi 71 wamefukuzwa kazi
katika vituo mbalimbali vya mizani hapa nchini kutokana na kujihusisha na vitendo
vya rushwa.
Ameongeza kuwa
TANROADS wamejipanga kuhakikisha miradi yote ya ujenzi na vituo vya mizani
vinafanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kujenga imani kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya
TANROADS Hawa Mmanga, amemuhakikishia Naibu Waziri wa Ujenzi kuwa wakala wake umejipanga
kutekeleza kikamilifu ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja hapa nchini
kwa wakati, ubora na kuzingatia thamani ya fedha.
Wajumbe
wa baraza la TANROADS kutoka mikoa yote
nchini wamekutana katika mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi ili kutathimini
utendaji kazi wao na kuibua mikakati mipya itakayowezesha wakala huo kufanya
kazi zake kwa weledi na kwa kukidhi mahitaji ya nchi.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Novemba 26,2017 katika kata 43 utagharimu Sh2.5 bilioni.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema msingi wa bajeti ya uchaguzi unategemea idadi ya vituo vya kupigia kura na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika kata husika.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari leo Novemba Mosi,2017 Kailima amesema idadi ya wapiga kura ndiyo inatoa bajeti ya mahitaji ya vifaa vya kuendeshea uchaguzi kama vile karatasi za kura na idadi ya vituo ambavyo vinakuwa na watumishi wasiopungua wanne.
Amesema kituo cha kupigia kura kina watendaji wanne ambao ni msimamizi na msimamizi msaidizi, karani mwongozaji na mlinzi wa kituo.
“Lakini pia kuna watu wa ziada kama wasimamizi wasaidizi wako ngazi ya kata na jimbo ambao wanahusika kusimamia uchaguzi katika maeneo husika,” amesema.
Amesema gharama nyingine za uchaguzi ziko kwenye usafirishaji wa vifaa kutoka Tume kwenda kwenye halmashauri husika na kutoka halmashauri kwenda kwenye kata ambako uchaguzi unafanyika. “Gharama hizo pia zinahusu utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia machapisho mbalimbali ya elimu ya mpiga kura, maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi,” amesema.
Amesema elimu pia hutolewa kupitia vyombo vya habari na machapisho yatakayotumika kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura.
“Kwa uchaguzi huu mdogo bajeti ni Sh2.5 bilioni. Si kwamba kila kata itatumia gharama sawa za fedha hizi, bali kuna kata itatumia Sh20 milioni kutokana na idadi ya vituo vya kupigia kura kuwa vichache na kata yenye vituo vingi kwenye uchaguzi huu itatumia Sh150 milioni,” amesema Kailima.
Kailima amesema vyama vya siasa vinatakiwa kuhakikisha vinawaelimisha wafuasi, wapenzi na wanachama wao juu ya kutekeleza maadili katika kipindi chote cha kampeni.
Amesema maadili yatakiukwa, chama husika pamoja na mgombea watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kailima amesema baadhi ya vitendo vya kuvunja maadili ya uchaguzi ni kuchana mabango ya wagombea, kutoa lugha chafu wakati wa mikutano ya kampeni na kupitisha muda wa kufanya mikutano ya kampeni.
Amesema kamati za maadili za kata na jimbo zitachukua hatua kali kwa chama au mgombea ambaye atakiuka maadili na kwamba, zinatakiwa kuchukua hatua ndani ya saa 48 baada ya chama au mgombea anapovunja maadili.
Amezitaja baadhi ya adhabu ni kuomba radhi wananchi hadharani, kutotumia vyombo vya habari kwa muda fulani wakati wa kampeni, onyo la maandishi, kusimamishwa kufanya kampeni, mgombea kutangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa yeye ni bingwa wa kukikuka maadili ya uchaguzi au kutozwa faini ya Sh100,000.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema msingi wa bajeti ya uchaguzi unategemea idadi ya vituo vya kupigia kura na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika kata husika.
![]() |
| Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani |
Katika taarifa kwa vyombo vya habari leo Novemba Mosi,2017 Kailima amesema idadi ya wapiga kura ndiyo inatoa bajeti ya mahitaji ya vifaa vya kuendeshea uchaguzi kama vile karatasi za kura na idadi ya vituo ambavyo vinakuwa na watumishi wasiopungua wanne.
Amesema kituo cha kupigia kura kina watendaji wanne ambao ni msimamizi na msimamizi msaidizi, karani mwongozaji na mlinzi wa kituo.
“Lakini pia kuna watu wa ziada kama wasimamizi wasaidizi wako ngazi ya kata na jimbo ambao wanahusika kusimamia uchaguzi katika maeneo husika,” amesema.
Amesema gharama nyingine za uchaguzi ziko kwenye usafirishaji wa vifaa kutoka Tume kwenda kwenye halmashauri husika na kutoka halmashauri kwenda kwenye kata ambako uchaguzi unafanyika. “Gharama hizo pia zinahusu utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia machapisho mbalimbali ya elimu ya mpiga kura, maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi,” amesema.
Amesema elimu pia hutolewa kupitia vyombo vya habari na machapisho yatakayotumika kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura.
“Kwa uchaguzi huu mdogo bajeti ni Sh2.5 bilioni. Si kwamba kila kata itatumia gharama sawa za fedha hizi, bali kuna kata itatumia Sh20 milioni kutokana na idadi ya vituo vya kupigia kura kuwa vichache na kata yenye vituo vingi kwenye uchaguzi huu itatumia Sh150 milioni,” amesema Kailima.
Kailima amesema vyama vya siasa vinatakiwa kuhakikisha vinawaelimisha wafuasi, wapenzi na wanachama wao juu ya kutekeleza maadili katika kipindi chote cha kampeni.
Amesema maadili yatakiukwa, chama husika pamoja na mgombea watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kailima amesema baadhi ya vitendo vya kuvunja maadili ya uchaguzi ni kuchana mabango ya wagombea, kutoa lugha chafu wakati wa mikutano ya kampeni na kupitisha muda wa kufanya mikutano ya kampeni.
Amesema kamati za maadili za kata na jimbo zitachukua hatua kali kwa chama au mgombea ambaye atakiuka maadili na kwamba, zinatakiwa kuchukua hatua ndani ya saa 48 baada ya chama au mgombea anapovunja maadili.
Amezitaja baadhi ya adhabu ni kuomba radhi wananchi hadharani, kutotumia vyombo vya habari kwa muda fulani wakati wa kampeni, onyo la maandishi, kusimamishwa kufanya kampeni, mgombea kutangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa yeye ni bingwa wa kukikuka maadili ya uchaguzi au kutozwa faini ya Sh100,000.
KANISA la Enjoying Assemblies of God linakukaribisha katika ibada zao zinazofanyika kila siku ya Jumapili Asubuhi hadi mchana, Jumatano saa 10:00 jioni na Ijumaa, Jumanne niwanawake (wanamama), Alhamisi saa 10:00 jioni ni Waimbaji.
Siku ya Ijumaa ni Maombi na maombezi.
Mito ya Injili Linawakaribisha watu wote.
Siku ya Ijumaa ni Maombi na maombezi.
Mito ya Injili Linawakaribisha watu wote.












