Habari Mpya

Habari Zote


·       Yamo kisukari, saratani, presha, hamu ya tendo

MMEA wa bamia uzaao matuda yanayoliwa, ni zao linalostawi karibu maeneo yote hapa nchini, ingawa hustawi na hupedwa zaidi na watu wa ukanda wa Pwani. Huliwa kama mboga kwa matunda hayo kupikwa yakichanganywa na aina nyingine ya mboga kama vile nyama.

Watu wa ukanda wa Pwani hutumia bamia kwa kuikatakata vipande vidogo na kuchanganya vipande hivyo na  majani ya maboga, magadi kisha kupika pamoja na kupata mboga iitwayo mlenda au hombwe kwa watu wa pwani ya mkoa wa Tanga.

Kwa bahati mbaya sana walaji wengi hawajui umuhimu wake kifya kama anavyobainisha Mtaalamu na Mkufunzi wa Chuo cha Tiba na Uuguzi ( IMTU) cha jijini Dar es salaam, Dk. Daniel Elifariji Mtango.

Mtaalamu huyo wa kitengo cha Afya na Jamii Chuoni hapo, anasema tunda la bamia lina vitamini A na B ambavyo huimarisha macho kutokana na  virutubisho hivyo kusheheni kiasi kingi cha protini ukilinganisha na lishe nyingine inayotokana na mimea.

Kama hiyo haitoshi, viini lishe vilivyomo husaidia kuwaokoa watoto  wenye  tatizo la utapiamlo, isulini kufanya kazi hivyo kuwaondoa watu katika hatari ya ugonjwa wa kisukari kwa  kuuweka sawa mfumo wa sukari mwilini.

Zinapoliwa kwa usahihi, huongeza kinga za mwili kwa watoto na watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka na kuwa kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine yanayosababishwa na kushuka kwa kinga ya mwili, anasema.

Akifafanua zaidi, Dk. Mtango anasema, maji ya bamia husaidia kuzuia magonjwa ya moyo kwa kuifanya mishipa ya damu kufanya kazi vizuri kutokana na maji yake kuwa  uwezo  wa kuondoa lehemu kwenye kuta za mishipa ya damu.

“Lehemu zisipoondolewa kwenye mishipa hiyo husababisha msukumo wa damu kwenda vibaya na kuwa chanzo cha maradhi ya shinikizo la damu. Kwa hiyo tunaona ni kwa jinsi gani ambavyo mmea huu ulivyo muhimu katika lishe na kudhibiti magonjwa ambayo wakati mwingine hayawezi kutibiwa hapa nchini. Hivyo bamia inaweza kupunguza idadi ya watu kwenda India kutibiwa maradhi ya moyo,”anasema,

Faida zingine za ulaji wa bamia  ni kuzuia tatizo la watoto kupasuka uti wa mgongo au mgongo waz, kumsaidia mama mjawazito pamoja na mtoto  tumboni  kuwa na afya  na baada ya kujifungua.
Hutibu tatizo la  kuchoka bila sababu, zaidi  kwa watu ambao wana msongo wa mawazo ambao mtaalamu anashauri kundi hilo kula kwa wingi bamia kwani huleta matokeo ya haraka na kufanya afya zao kuimarika zaidi na kuwafanya  wawe na amani, furaha muda wote.

Faida nyingine, hutibu vidonda vya tumbo na kuthibiti bakteria  wasababishao matatizo hayo na kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo, huongeza kiwango cha uzalishaji wa damu kwa wingi mwilini.

Huimarisha nywele na kuzifanya ziwe na muonekano mzuri pamoja na kufanya utumbo mpana kubaki katika ulaini wa asili yake  na kukinga mtumiaji dhidi ya  saratani ya utumbo mpana (large intestine).

Pia hufanya mfumo wa usagaji wa chakula kuwa mzuri na hivyo kupunguza maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa kutokana na majimaji ya bamia hulainisha choo kama ilivyo papai na ndizi mbivu. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa.

MATUMIZI:
·         Mlaji anaweza kupika bamia kama mboga kisha kuchanganya na chakula kingine na kula kama mlo. Vyakula hivyo vinaweza kuwa, uji, mchuzi, na vingine.

·         Matumizi mengine ni mtumiaji anatakiwa kukatakata bamia vipande vidogovidogo baada ya kuoshwa kwa maji safi na salama. Loweka kwenye maji kwa dakika kadhaa vipande hivyo kulingana na uwingi wa vipande vyenyewe ili kupata juisi.

·         Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha juisi ya bamia sawa na gramu 100. Au unaweza kula vipande hivyo vibichi vilivyojazwa kwenye kikombe cha ujazo huo .

·         Inashauriwa kuwa watoto wadogo wapatiwe  zikiwa zimepikwa.  Fanya hatua hizo tatu kwa mfululizo na matokeo yake hujitokeza kuanzia juma la tatu au kabla.


Anatoa ushauri kwa wakulima kulima zao hilo kwa wingi kutokana na faida hizo za kiafya na kukifanya kilimo chao kuwa na tija.

Ni zao linalokomaa kwa muda mfupi na hukabiliana na hali zote za hewa. Pia jamii kula kwa wingi bamia ili kupunguza matatizo ya kiafya  ambayo baadhi yake ameyaanisha katika makala haya.
WANAFUNZI wawili wa shule ya msingi Sarawe iliyoko katika tarafa ya Chamriho halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara, wamekufa na wengine sita kujeruhiwa katika ajali mbaya ya kuangukiwa ukuta wa chumba cha darasa wakati wakipembua mahindi kwa ajili ya chakula chao shuleni hapo.

 Tukio hilo limetokea juzi majira saa kumi jioni wakati wa saa ya mapumziko katika eneo la shule hiyo.

 Wanafunzi waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na Anastazia Wazilana (8) aliyekufa papo hapo na Amosi Stima Igala (8) aliyekufa wakati akikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu zaidi, ambapo wote walikuwa wanasoma darasa la pili shuleni hapo.
 Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Dk. Nuru Yunge amethibitisha vifo hivyo na kwamba majeruhi walipelekwa kituo cha afya Ikizu na wengine wamehamishiwa katika hospitali ya DDH Bunda.

 “Pale kituo cha afya Ikizu tulipokea majeruhi saba, na wengine wawili tukawahamishia katika hospitali ya DDH Bunda, kutokana na hali zao kuwa mbaya, lakini kwa taarifa niliyopata majeruhi mmoja amekufa wakati akipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando” alisema.

 Afisa tarafa ya Chamriho Boniphace Maiga, aliwataja wanafunzi waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Happynes Mussa (13) wa darasa la tano, Wambura Nyamrosha (12) wa darasa la nne, Sara Wazilana (14) wa darasa la sita, Emmanuel Mkiriti (8) wa darasa la pili, Mugaya Galinde (8) wa darasa la pili na Pili Juma Matwiga (7) wa darasa la kwanza.

 Maiga alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni ukuta wa darasa hilo kuwa na ufa wa siku nyingi, ambapo uliporomoka na kuwaangukia wakati wakianda mahindi kwa ajili ya chakula cha wanafunzi shuleni hapo, kinachotolewa na shirika la PCI.

 “Wakati wa mapumziko wanafunzi hao walikuwa nje ya dasrasa hilo wakipembua mahindi ya PCI na ghafla ukuta huo ulidondoka na ulikuwa na naufa mkubwa siku ninyingi. Mwanafunzi mmoja alifia hapo hapo na mwengine amekufa wakati akikimbizwa Bugano baada ya kuwapatiua rufa.

 Baadhi ya mashuhuda akiwemo katibu wa huduma za jamii katika serikali ya kijiji cha Sarawe, Richard Karangi, walilielezea tukio hilo kuwa ni la kusikitisha, ambapo muuguzi mmoja katika hospitali ya DDH Bunda, alizungumzia hali ya majeruhi mmoja aliyempokea kwamba inaendelea vizuri.

 Kamanda wa polisi mkoani Mara kamishina msaidizi wa polis, Jafari Mohamed hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini polisi wilayani hapa wamethimitisha kuwepo kwa tukio hilo.


 Wakati huo huo, baadhi ya wananchi waliozungumza na waandishi wa habari walisema kuwa ipo haja ya wakaguzi wa shule kukagua majengo ambayo hayana ubora na kuagiza yasitumiwe na wanafunzi ili kuepusha majanga kama hayo  ambayo siyo ya lazima yasitoke tena.
BOGA ni moja kati ya matunda yenye faida mbalimbali katika mwili wa binadamu. Hupatikana karibu mikoa yote ya Tanzania, na idadi kubwa ya watu wengi kulima boga kwa matumizi ya nyumbani kama chakula.

Wengi pia hawajui faida za tunda zaidi ya kulitumia kama chakula, lakini ukweli ni kwamba matumizi yake ni zaidi ya chakula.

Boga huweza kusindikwa au kusagwa na kupatikana kimiminika (juisi) muhimu kwa afya ya binadamu kwani hutibu magonjwa mbalimbali.

Dk. Othman Shemu ni mtaalamu wa miti na mimea dawa na Mkurugenzi mtendaji wa kliniki ya tiba asili cha Paseko yenye makao yake Tabata relini Jijini Dar es Salaam, anasema juisi ya boga pia huimarisha na kuongeza nguvu za kiume.

Huwafanya wanaume kumudu tendo la ndoa hasa wale ambao huishia mshindo au pigo moja au kushindwa kumfikisha kileleni mwanamke na wakati mwingine kukosa hamu ya tendo la ndoa Anasema tunda la boga lina protini na virutubisho mbalimbali vyenye uwezo wa kutibu magonjwa ikiwamo kutengeneza mbegu za kiume kwa wingi kama ilivyo baadhi ya vyakula vya protini.

Baadhi ya magonjwa hayo ni tezi dume, kusafisha figo, tatizo la kutapika mfululizo hasa kwa mama mjamzito, huondoa tatizo ya gesi tumboni na msongo wa mawazo.
“Ukitunia juisi hii huruhusu ubongo kuingiza hewa safi kwa wingi (oxgen) na kutoa hewa chafu hali inayofanya ubongo kuwa mwepesi na kutunza kumbukumbu za kutosha, “ anasema Dk Shemu.

Pia huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni na kuondoa vijidudu visivyotakiwa tumboni, pamoja na kusaidia kurekebisha mfumo wa msukumo wa damu kwa watu wenye matatizo ya presha.

Huweza kutumiwa na rika za watu wote ingawa ni muhimu zaidi kutumiwa na watoto kwani huwakinga na magonjwa na kuwasaidia kujenga uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu (akili) jambo ambalo linaweza kuongeza ustawi wa masomo darasani.
UANDAAJI:

Shemu ambaye pia ni katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Waganga (SHIVYATIATA) anasema zipo njia mbalimbali za uandaaji wa ambapo mhussika anasema kumenya maganda ya juu yasiyotakiwa kisha maandalizi kuanzia nyama (sehemu ya njano), moyo na mbegu.

Chukua nyama, kata vipande vidovidogo baada ya kusafishwa kwa maji safi na salama. Jaza vipande hivyo kwenye mashine maarufu kama (Brenda) kwa ajili ya kusaga au kusindika.

Unaweza wakati wa kusindika unaweza kuchanganya vipande hivyo na ndizi, maji safi kidogo ili kurahisisha usindikaji kutokana na ndizi na vipande vya boga kuwa katika hali kavu.

Inashauriwa kuwa juisi iliyosindikwa katika mchanganyiko huo ina ongezeko kubwa la virutubisho kama vile kalishiamu husaidia watu wenye upungufu au ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI) kuongeza kinga ya mwili.

“Pia majaribio yetu yameonyesha kwamba juisi hii ikichanganywa na juisi ya maua yajulikanayo kama rosemary maarufu kama rosella inakuwa na uwezo zaidi katika tiba kutokana na virutubisho vingine kama kalishiam na magnesiamu vilivyomo kwenye rosella,”alisema.

Zipo aina mbalimbali za uandaji wa juisi ya boga kwa mtu mwenye tatizo la nguvu za kiume hutakiwa, kuchukua boga na kulikata vipande vidogo vidogo na kusaga bila vipande hivyo kuwa mbegu zake.

Anachotakiwa mhusika kufanya ni kuzipaa mbegu za boga ili kuzitenganisha na nyama kisha kuzianika sehemu yenye kivuli hadi zitakaponyauka, saga kwa ajili ya kupata unga.

Inashauriwa kusaga unga huo wakati wa matumizi tu kwani unga wake ukihifadhiwa muda mrefu unaweza kusababisha mlundikano wa fangasi ambao ni hatari kiafya, alisema Dk. Shemu.

MATUMIZI:
Unaweza kunywa juisi ya boga iliyosindikwa na kuchanganywa na pensheni ili kuongeza ladha (test) na sukari kidogo kadri unavyoweza kwasababu matumizi yake mengi hayadhuru.

Kuhusu unga wa mbegu za boga, mtumiaji mwenye matatizo hayo anatakiwa kuchukua unga kwenye kijiko kimoja cha chai kisha kuchanganya kwenye glasi ya maji na kunywa.


“Kunywa mara tatu kwa siku. Mwneye tatizo kubwa anapaswa kunywa katika muda wa siku 21 mfululizo. Kwa mwenye tatizo la msongo wa mawazo anaweza pia kunywa juisi ya mchanganyiko wa ndizi mbivu na boga kwa kuchanganya na unga wa mbegu hizo”alisema.
TANZANIA imezidi kupata neema kutoka Jumuiya ya Kimataifa ambapo Novemba 2, 2017, Umoja wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 50, takriban Shilingi bilioni 130 kwa ajili ya kufadhili Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban (kushoto) akiupokea ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya, ukiongozwa na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo Neven Mimica (katikati) na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Roeland van de Geer, walipokuwa wanawasili Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa msaada wa Euro milioni 50 kwa Tanzania.

Mkataba wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Neven Mimica.


Msaada huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya nishati ya umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao wa usambazaji umeme.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu wake.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (kulia) na akimweleza jambo Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Neven Mimica wakati wa hafla fupi ya Umoja wa Ulaya (EU) kutiliana saini makubaliano ya msaada wa Euro milioni 50 kwa ajili ya kusaidia usambazi wa umeme vijijini kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza umeme Vijijini (REA).
“Umoja wa ulaya ni wadau wetu muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu na mikubwa wanayotupatia, na kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema  James

Alisema kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo bila masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya viwanda itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akitoa maelezo ya ujio wa ugeni huo kuwa ni neema kwa nchi ya Tanzania kwani Umoja wa Ulaya wametoa msaada wa Euro Milioni 50 utasaidia vijijini 3600 nchini kupata  umeme.

Doto James alisema kuwa tangu Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini REA uanze miaka 9 iliyopita, idadi ya vijiji vilivyounganishiwa umeme imeongezeka kutoka vijiji 400 mwaka 2008 hadi kufikia vijiji 4395 hivi sasa.

Alisema kuwa ni matarajio ya Serikali kwamba ifikapo mwaka 2020, vijiji vyote 12,000 hapa nchini vitakuwa vimeunganishwa na nishati hiyo hivyo kuchochea shughuli za uzalishaji viwandani na kiuchumi kwa wananchi, vitaimarika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akiagana na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Neven Mimica, baada ya kusaini mkataba wa msaada wa Euro milioni 50 ambazo Umoja huo umeipatia Tanzania kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini REA.

Kwa upande wake, Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Neven Mimica, amesema kuwa msaada huo wa Euro milioni 50 wanaoutoa ni sehemu ya msaada wa Euro milioni 207 ambazo wanachama wengine wa Umoja huo, ikiwemo Sweden, Uingereza, Norway na Benki ya Dunia, watatoa kufanikisha mradi huo wa usambazaji umeme vijijini kupitia REA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akiwa na Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa msaada wa utekelezaji wa nishati ya umeme vijijini katika ukumbi wa Wizara ya fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam


“Nguvu hizi za pamoja zitaviwezesha takriban vijiji 3,600 vilivyoko maeneo mbalimbali ya nchi ambapo watu zaidi ya milioni 1 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo” Alisema
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akiwa pamoja na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Neven Mimica wakisaini Mkataba wa  msaada wa fedha za kusaidia usambazaji wa umeme Vijijini (EURO milioni 50) katika ukumbi wa  Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Alisema hatua hiyo itachangia kuimarika kwa ubora wa maisha ya wananchi wa Tanzania, kuimarika kwa sekta za afya, elimu na kuleta faida za kijamii na kiuchumi zinazoonekana kwao moja kwa moja hususan wanawake na watoto.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya Neven Mimica, wakibadilishana hati za makubaliano ya msaada wa ruzuku ya kiasi cha EURO Milioni 50 katika ukumbi wa wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Misaada ya Umoja wa Ulaya kwa Tanzania imejikita katika Nyanja tatu za Utawala bora, Umeme na Kilimo endelevu ambapo Umoja huo kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (EDF) umetenga kiasi cha Euro milioni 626 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014-2020
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (Mb), amewapongeza Wakala wa barabara nchini (TANROADS), kwa mikakati wanayotumia kudhibiti vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini.

Akifungua Mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi la TANROADS mjini Kigoma, Kwandikwa, amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watendaji wake wote wanakuwa waadilifu ili rasilimali chache zitumike kwa manufaa ya wote.

“Hakikisheni kila mtakaye mkamata kwa vitedo vya rushwa hatua za kisheria anachukuliwa ikiwemo na kufukuzwa kazi ili kuonyesha kuwa jambo la rushwa tunalichukia na hatulipendi katika Serikali”, alisema.

Naye Mtendaji Mkuu Wa Wakala huo Eng. Patrick Mfugale, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja watumishi 71  wamefukuzwa kazi katika vituo mbalimbali vya mizani hapa nchini kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Ameongeza kuwa TANROADS wamejipanga kuhakikisha miradi yote ya ujenzi na vituo vya mizani vinafanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kujenga imani kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS Hawa Mmanga, amemuhakikishia Naibu Waziri wa Ujenzi kuwa wakala wake umejipanga kutekeleza kikamilifu ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja hapa nchini kwa wakati, ubora na kuzingatia thamani ya fedha.


Wajumbe wa baraza la TANROADS kutoka mikoa yote  nchini wamekutana katika mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi ili kutathimini utendaji kazi wao na kuibua mikakati mipya itakayowezesha wakala huo kufanya kazi zake kwa weledi na kwa kukidhi mahitaji ya nchi.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Novemba 26,2017 katika kata 43 utagharimu Sh2.5 bilioni.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema msingi wa bajeti ya uchaguzi unategemea idadi ya vituo vya kupigia kura na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika kata husika.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani

Katika taarifa kwa vyombo vya habari leo Novemba Mosi,2017 Kailima amesema idadi ya wapiga kura ndiyo inatoa bajeti ya mahitaji ya vifaa vya kuendeshea uchaguzi kama vile karatasi za kura na idadi ya vituo ambavyo vinakuwa na watumishi wasiopungua wanne.

Amesema kituo cha kupigia kura kina watendaji wanne ambao ni msimamizi na msimamizi msaidizi, karani mwongozaji na mlinzi wa kituo.

“Lakini pia kuna watu wa ziada kama wasimamizi wasaidizi wako ngazi ya kata na jimbo ambao wanahusika kusimamia uchaguzi katika maeneo husika,” amesema.

Amesema gharama nyingine za uchaguzi ziko kwenye usafirishaji wa vifaa kutoka Tume kwenda kwenye halmashauri husika na kutoka halmashauri kwenda kwenye kata ambako uchaguzi unafanyika.  “Gharama hizo pia zinahusu utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia machapisho mbalimbali ya elimu ya mpiga kura, maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi,” amesema.

Amesema elimu pia hutolewa kupitia vyombo vya habari na machapisho yatakayotumika kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura.

“Kwa uchaguzi huu mdogo bajeti ni Sh2.5 bilioni. Si kwamba kila kata itatumia gharama sawa za fedha hizi, bali kuna kata itatumia Sh20 milioni kutokana na idadi ya vituo vya kupigia kura kuwa vichache na kata yenye vituo vingi kwenye uchaguzi huu itatumia Sh150 milioni,” amesema Kailima.
Kailima amesema vyama vya siasa vinatakiwa kuhakikisha vinawaelimisha wafuasi, wapenzi na wanachama wao juu ya kutekeleza maadili katika kipindi chote cha kampeni.

Amesema maadili yatakiukwa, chama husika pamoja na mgombea watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kailima amesema baadhi ya vitendo vya kuvunja maadili ya uchaguzi ni kuchana mabango ya wagombea, kutoa lugha chafu wakati wa mikutano ya kampeni na kupitisha muda wa kufanya mikutano ya kampeni.

Amesema kamati za maadili za kata na jimbo zitachukua hatua kali kwa chama au mgombea ambaye atakiuka maadili na kwamba, zinatakiwa kuchukua hatua ndani ya saa 48 baada ya chama au mgombea anapovunja maadili.

Amezitaja baadhi ya adhabu ni kuomba radhi wananchi hadharani, kutotumia vyombo vya habari kwa muda fulani wakati wa kampeni, onyo la maandishi, kusimamishwa kufanya kampeni, mgombea kutangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa yeye ni bingwa wa kukikuka maadili ya uchaguzi au kutozwa faini ya Sh100,000.

KANISA la Enjoying Assemblies of God linakukaribisha katika ibada zao zinazofanyika kila siku ya Jumapili Asubuhi hadi mchana, Jumatano saa 10:00 jioni na Ijumaa, Jumanne niwanawake (wanamama), Alhamisi saa 10:00 jioni ni Waimbaji.

Siku ya Ijumaa ni Maombi na maombezi.

Mito ya Injili Linawakaribisha watu wote.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amekagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na yakisasa itakayotoa huduma za usafirishaji katika  Ziwa Victoria.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi,akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa(Wa pili kulia), hatua zilizofikiwa za ukarabati wa meli ya Mv. Clarius na Mv. Umojakatika Bandari ya Mwanza.

Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Prof. Mbarawa, amewataka wafanyakazi wa Kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili kazi hiyo ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.

“Mkandarasi ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki wa kimahesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na muda mfupi”, amesema Prof. Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa, amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya Mv. Clarias na Mv. Umoja ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa, na hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Bandari  ya “Port Bell”, nchini Uganda.

“Kukamilika kwa meli kuwiane na kasi ya kutafuta mzigo mwingi ili meli hizi zifanye biashara wakati wote na kuhakikisha Kampuni yenu inapata mapato mengi yatakayowawezesha kujiendesha kwa faida”, amesisitiza Waziri Mbarawa

Naye, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Erick Hamissi, amemhakikishia Prof. Mbarawa, kuwa wamejipanga kufanya ukarabati mkubwa wa meli za Mv. Victoria, Butiama na Liemba ili kuziwezesha meli hizo kufanya kazi katika ubora wake wa awali na kupunguza tatizo la usafiri katika ziwa Victoria na Tanganyika.

“Tumeweka mkakati wa kuhakikisha tunazikarabati meli zetu zote ili ziwe katika ubora unaostahili wakati wote”, amefafanua Bw. Hamissi.

Katika kuhakikisha maendeleo ya kibiashara na kuichumi  yanafikiwa katika Ukanda wa maziwa makuu  nchini, Serikali imejipanga kuhakikisha inafufua usafiri wa meli za abiri na mizigo katika ukanda huo.
TUME ya uchaguzi imeahirisha uchaguzi katika kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay.
Vituo vya kura katika baadhi ya maeneo tayari vimefungwa.

Kinyume na uchaguzi wa mwezi Agosti, katika vituo vya kupigia kura hakukuwa na foleni ndefu.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesusia uchaguzi huo na kuwataka wafuasi wake wasalie manyumbani

Uchaguzi huu unatokana na hatua ya Mahakama ya Juu kufuta uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti

UCHAGUZI NI VURUGU KENYE

HOSPITALI ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo, haina chumba cha kuwalaza wagonjwa mahututi (ICU) hali inayosababisha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa matibabu, hulazimsihwa kuwekwa katika wodi za wagonjwa wengine, wakiwa na mitungi ya mashine za gesi za kupumulia.
 
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo
Uchunguzi uliofanywa na Majira takribani mwezi mmoja katika hospitali hiyo ya rufaa inayopokea wagonjwa kutoka katika vituo vya afya na hospitali za wilaya nane zilizopo mkoani hapa, na kuthibitishwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga (RAS) Injinia Zenna Said, Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga, Dk. Asha Mahita na Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Jumanne Karia kwa pamoja walielezea jitihada za mkoa za kuhakikisha wanajenga chumba hicho.

Hospitali hiyo kongwe hapa nchini, imekuwa na tatizo hilo takribani miaka 7 sasa, kwa chumba hicho kukosekana ambapo awali walikuwa wakitumia chumba kimoja kabla ya kusitisha kualza wagonjwa, kikawa kinatumiwa na watoto wadogo lakini baadaye kikawa kinatumiwa na wagonjwa wanaotumia kadi za huduma ya Bima ya Afya, lakini sasa kinatumika kwa shughuli nyingine za hospitali.

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga, wamekuwa wakilalamikia hali hiyo wakieleza kwamba wagonjwa Mahututi kuwachanganya na wagonjwa wengine huku wakiwa na mitungi ya gesi ni kutowatendea haki, kwa kuwa wanaporuhusiwa ndugu kuona wagonjwa kunakuwa na msongamano mkubwa na kelele za hapa na pale za kufariji wagonjwa wengine.

“Nilishtuka nilipoingia wodi ya Galanosi kule kwa akina mama nilimkuta mke wa diwani wa Kirare, Saleh Mwagilo akiwa amewekewa mashine ya gesi huku akiwa mahututi, nilishangaa nilipouliza nikaambiwa hospitali haina chumba cha wagonjwa mahututi,” alisema Haruna Magembe aliyekuwa na mgonjwa katika wodi hiyo ya Galanosi.

Alisema kuwa licha ya kuwepo mgonjwa huyo katika wodi nyingine mbalimbali zimekuwa na wagonjwa mahututi wengi wanaochanganywa na wagonjwa wa kawaida haliambayo imekuwa ikileta tafsiri mbaya ya suala la viongozi wa mkoa kuwajibika katika kuhakikisha chumba hicho kinapatikana ili kuwawezesha wagonjwa hao kupata tiba stahili kwa mujibu wa taratibu na sera ya wizara ya afya.

Alipotafutwa diwani huyo kwa ajili ya kuelezea suala la mgonjwa wake huyo, hakuweza kupatikana lakini mtu wake wa karibu aliyejitambulisha kwa jina la Kasirani kasirani, alisema amemhamishia mkewe huyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako anaendelea na matibabu baada ya kulazwa takribani wiki mbili akiwa na mtungi wa oksijeni bila mafanikio.

Alipoulizwa kuhusu hali hiyo Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Injinia Zena alikiri kukosekana kwa chumba hicho, lakini alisema kwa taarifa za jitihada zinazofanyika kupata chumba hicho, alimwelekeza mwandishi wa habari hizi akakutane na Mganga Mkuu wa mkoa Mahita ambaye atakuwa na majibu kuhusu kukosekana kwa ICU katika hospitali hiyo.

“Ni kweli lakini sisi kama mkoa tumekuwa na mipango mbalimbali ya kupatikana lakini nenda kwa Mganga Mkuu atakupa tumefikia wapi kuhusu kupatikana kwa ICU,” alisema Injinia Zenna.

Dk. Mahita alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema kuwa ni kweli hawana ICU katika hospitali hiyo lakini wagonjwa wenye mahitaji hayo wamekuwa wakiwahudumia vizuri licha ya kukosa chumba kinachofaa kwa huduma hiyo na kwamba hawawezi kuwazuia watu wanaokuja kuwaona wagonjwa waliowachanganya na wagonjwa wengine.

Hata hivyo, Dk Mahita ambaye alisema pamoja na kukosa huduma hiyo hospitali hiyo katika kipindi cha hivi karibuni wameweza kuboresha huduma mbalimbali na kuhusu ICU wamekuwa na jitihada mbalimbali za kuhakikisha wanamaliza tatizo hilo baada ya kuomba mkopo kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

“Tumeomba mkopo NHIF kwa ajili ya ICU, lakini kwa sasa wagonjwa wanaokuja kwa mahitaji ya huduma ya ICU tunawapa huduma, tunachokosa ni eneo la kutolea huduma hiyo tu,” alisema na kuongeza “Hatuwezi kuwazuia watu wasiende kutazama wagonjwa wao waliokuwa na oksijeni, lakini ukitaka taarifa zaidi nenda kamuone Dk. Karia ambaye ni Mganga Mfawidhi wa hospitali, atakupa hadi sasa tumefikia wapi katika suala hilo,”.

Akizungumzia kuhusu hali hiyo Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Karia alisema kuwa ni kweli chumba hicho kwa sasa hakipo katika hospitali hiyo baada ya chumba kilichokuwa kikitumika zamani hakina mfumo wa kutumia gesi pamoja na vifaa vya ICU, hivyo wakaamua kuwachanganya wagonjwa wenye mahitaji hayo na wagonjwa wengine, lakini tangu mwaka 2013 wameanza ukarabati wa jengo ambalo litatumika kwa huduma hiyo.

Alisema chumba wanachokifanyia ukarabati sasa ili kitumike kuwa ICU ni kile kilichokuwa kikitumika kama chumba cha Upasuaji (Theatre) baada ya mradi wa KfW kutoa fedha za ujenzi wa chumba cha Upasuaji kipya kinachotumika sasa na kwamba sasa wanaendelea kutafuta fedha ili waweze kukamilisha katika kipindi kifupi kijacho.

“Ni kweli kile chumba cha mwanzo kilichokuwa kikitumika kama ICU hatukitumii tena na tunachanganya wagonjwa huko katika mawodi, lakini chumba kile kilikuwa hakina mfumo wa gesi, pia hakikuwa na vifaa vinavyohitajika kwa wagonjwa mahututi ikiwemo vitanda,” alisema Dkt Karia.

Aliongeza kusema kwamba katika bajeti yam waka 2017/2018 itatumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ICU na kiasi cha shilingi milioni 231 ilitengwa mwaka 2016/2017 kwa jili ya kutengeneza mfumo wa gesi katika chumba hicho ambapo hospitali kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Tawala, imeanza kushughulikia suala hilo la gesi ambayo pia wataiuza katika hospitali nyingine baada ya kuanza kazi.

“Vile vile kuna vifaa vya msaada kutoka nchini Ujerumani Mwenyekiti wetu wa bodi ya Hospitali Zahra Noor kwa kushirikiana na kaka yake Habib Noor na baadhi ya wafanyabiashara wa hapa Tanga akiwemo Selemani Rahaleo, watasaidia hiyo ICU yetu ikianza kazi,” alisema Dkt Karia na kuongeza kwamba wameomba mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 560 kutoka NHIF.

Akizungumza na gazeti hili Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afy (NHIF) mkoani Tanga, Ali Mwakababu alisema ni kweli hospitali hiyo imeomba mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 560 kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya akina mama na watoto pamoja na chumba cha magonjwa mahututi (ICU).

“Tutawapa mkopo wao huo, bahati nzuri mradi wao huo wa ICU umepitiwa hivi karibuni na Mwenyekiti wetu wa Bodi Mama Anna Makinda hivyo ni matumaini yetu kwamba watapewa wakati wowote fedha hizo ili kufanikisha suala hilo,” alisema Mwakababu na kuongeza kwamba mfumo wao hospitali hiyo inakopesheka kwa vile kwa mwezi huwa wanawalipa zaidi ya shilingi milioni 200 wanazotoa matibabu kwa wanachama wao.
SERIKALI inatarajia kuajiri wafanyakazi 400 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi kifupi kijacho ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa watumishi katika Mamlaka hayo, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi na makusanyo ya kodi.



Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wengine wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga, alipofanya ziara ya kikazi kukagua namna Mamlaka hayo inavyokusanya kodi.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga kuhusu kufanya juhudi ya kukusanya mapato ili azma ya Serikali ya kuwahudumia wananchi kikamilifu itimie.

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Shinyanga na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, alipokuwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji wa Mamlaka hayo mkoani humo.

Dk. Kijaji amesema kuwa taratibu zote zimekamilika na wakati wowote nafasi za ajira zitatangazwa na kwamba nafasi hizo zimelenga kuiwezesha TRA kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga kuhusu kufanya juhudi ya kukusanya mapato ili azma ya Serikali ya kuwahudumia wananchi kikamilifu itimie.
“Tunatambua changamoto ya uchache wa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ndio maana tumeamua kuajiri wafanyakazi hao 400 ambao ni wengi kuliko kada nyingine ili tuweze kuimarisha utendajikazi wa Mamlaka na hivyo kuongeza makusanyo ya kodi zinazotakiwa kwa shughuli za maendeleo nchini” alisema .

Alisema kuwa pamoja na uhaba wa watumishi, anaamini kuwa lengo la mwaka huu la kukusanya shilingi trilioni 17 ambazo Mamlaka hayo imepangiwa yatafikiwa na ikiwezekana kuzidi kwa kutumia wafanyakazi waliopo.

Dk. Kijaji alitoa rai kwa wafanyakazi wa TRA kuwa waadilifu na kwamba atakayebainika kukiuka maadili yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria.

Awali Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson, alieleza kuwa mkoa wake umepangiwa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 18 na kwamba wanauhakika wa kufikia lengo hilo kutokana na mikakati mbalimbali waliyojipangia ikiwemo kusimamia ukusanyaji kodi kikamilifu katika sekta ya madini.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Beatus Nchota alisema kuwa Mamlaka yake imejiwekea mipango ya kufungua ofisi zake kila wilaya hapa nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili lengo walilopewa la kukusanya shilingi trilioni 17 liweze kufikiwa.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, alisema kuwa Serikali mkoani humo itahakikisha kuwa TRA inatimiza malengo yake ya kukusanya kodi na kumhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji kwamba watasimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimetoa mkono wa pole kwa familia iliyopata ajali ya kuungua moto nyumba na kusababisha vifo vya watu wanne huko katika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla  Mabodi wakati wa kuifariji familia hiyo amesema CCM Zanzibar imesikitishwa sana na tukio hilo kwani limegharimu maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia.
 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu wa familia iliyopata msiba huo katika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
 Dk. Mabodi alisema kwa niaba ya Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  anatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo na kuwasihi waendelee kuwa  na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba huo.
“ Kupoteza watu  Wanne katika familia moja  ni jambo zito linalotia huzuni lakini tuendelee kuwa wavumilivu kwani Allah amewapenda zaidi na sisi tuliobaki tuendelee kuwaombea  dua ili wapate makaazi mema na kusamehewa madhambi yao”, alitoa nasaha hizo kwa maskitiko makubwa Dk. Mabodi.”
Mapema Sheha wa Shehia ya Fumba, Mohamed Suleiman alifafanua kuwa nyumba hiyo ilianza kuwaka moto majira ya saa 6:15 usiku Oktoba 21 mwaka huu, ambapo wananchi mbali mbali walianza juhudi za kuzima moto huo na kushindwa kuokoa watu waliokuwa ndani kwani uliku ni mkubwa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi  Akisalimiana na baadhi ya wananchi na viongozi mbali mbali walioudhuria katika msiba huo.
Suleiman alisema wakati juhudi za kuzima moto huo zikiendelea waliwasiliana na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar ambacho kilifika na kusaidiana na wananchi hao ambapo walizima moto huo na kukuta watu wanne tayari wamefariki dunia.
Akithibitisha tukio tukio hiloalisema chanzo cha moto huo ni hitilafu za umeme zilizoanzia katika waya wa jokofu (Friji) lililokuwa likifanya kazi wakati wa usiku.
Kamanda Nassir aliwataja watu waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Bahati Ali Ameir (40), Sinawema Abdalla Ali, Hashim Abdalla Ali (6) na Latifa Mohamed Ali (8).

Alitoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuzima vifaa vya umeme wakati wa usiku ambavyo havina umuhimu wa kutumiwa wakati huo ili kuepuka majanga yanayoweza kuhatarisha maisha ya watu.

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -