IMEELEZWA kuwa Wananchi wengi katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wamejenga Nyumba zao za kuishi bila ya kuwa na vibali maalumu vya ...
IMEELEZWA kuwa
Wananchi wengi katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wamejenga Nyumba zao za
kuishi bila ya kuwa na vibali maalumu vya ujenzi
kutoka katika Mamlaka husika za Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula |
Hali hiyo
imesababisha ujenzi holela katika Mji wa Kahama kwani Mamlaka husika imekuwa
haichukui hatua za Kisheria kwa Wananchi ambao wamekuwa wakifanya ujenzi huo
kinyume na Sheria na taratibu za ardhi zinavyosema.
Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Agelina Mabula aliyasema hayo juzi wakati
akipokea taarifa ya shughuli za Maendeleo za Wilaya ya Kahama na kuongeza watu
wanaofanya vitendo hicho lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Mabula alisema
kuwa kutokana na ujenzi huo wabila ya kuwa na vibali unasababisha kuwepo na
migongano pale uvunjaji wa nyumba unapotakiwa kufanyika ili
kupisha shughuli za maendeleo katika maeneo hayo.
Alisema kuwa kwa
sasa lazima kila kiongozi wa Serikali na Halmashauri kwa ujumla
kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria za mipango mji ili
kila takae taka kujenga awena kibali kutoka mamlaka na kuongeza kuwa
zoezi hilo sii kwa Wilaya ya Kahama tuu bali ni kwa nchi nzima.
“Nawaomba
Viongozi mhakikishe kuwa mnasimamia sheria na taratibu za
mipango miji katika maeneo yenu na agizo hili sii kwa viongozi wa Wilaya ya
Kahama tuu bali kwa viongozi wote wanchi nzima”, Alisema Angelina Mabula.
Hata hivyo
Mabula alisema kuwa Kahama wametia hasara Shirikal la Nyumba la Taifa (NHC) kwa
kutonunua nyumba zilizojengwa na shirika hilo tangu zilipojengwa miaka mitatu
iliyopita huku nyumba moja tuu kununuliwa kati ya nyumba 50.
Alisema kuwa
kutokana na hali ya kutonunuliwa nyumba hizo Naibu Waziri huyo alitoa Maagizo
kwa viongozi wa shirika hilo la nyumba kuhakikisha kuwa nyumba hizo zinauzwa
bila ya kujali kwa watumishi wa serikali au Wananchi ambao wameonyesha
kuzihitaji.
Mabula aliutaka
uongozi wa Shirika hilo la Nyumba Mkoa wa Shinyanga wasijikite kwa watumishiwa
serikali bali waangalie na watu wengine wanaohitaji nakuongeza kama
itashindikana kwa hilo basi nyumba hizo zipangishwe ili kuingiza fedha shirika
hilo.
Nyumba hizo za
Shirika la Nyumba zilijengwa takribani miaka mitatu iliyopita katika eneo la
zongomela Wilayani Kahama kwaajili ya kuziuza kwa Watumisi wa serikali lakini
mpaka kufikia sasa ni numba moja tuu kati ya 50 ndio imeweza
kununuliwa huku sababu kubwa ya kutopata wateja ikielezwa kuwa nibei kubwa.
Katika hatua
nyingine Angelina
alisema kuwa jumla ya Vijiji 112 vilivyopo katika Halmashauri ya shetu Wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga havijaingizwa bado katika mpango wa
matumizi bora ya ardhi Vijijini.
Kutokana na hali
hiyo ya kutoweka mpango kunasababisha kuwepo kwa uonevu baina ya ya serikali na
wananchi hali ambayo kwa sasa hata kama si vijiji vyote kuinginzwa basi angalau
hata vitano viwe katika mpango huo.
Alisema kwa
sasakuna baadhi ya Vijiji vina fedha kwa ajili ya kupimiwa aridhi na
kungeza kuwa kwa kushirikina na Wizara yake ataleta wataalamu kwaajili ya
kuwafundisha wananchi juu ya kuona umuhimu wa kupima viwanja.
Hata hivyo Naibu
Waziri huyo alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Michael Matomora
kuhakikisha wanawapimia Wananchi wa Ushetu vipande vya maeneo
yao ili waweze kupata hati miliki za kimila.
Aliendelea
kusema kuwa kwa sasa hata taasisi za kifedha zinatambua hati hizo ambazo
huwasaidia katika kupata mikopo mbalimbali ambo itawasaidia katika maendeleo ya
kimaisha hali ambayo itaweza kuleta mabadiliko ya kimaisha.
Mabula alisema
pia baadhi ya Viwanja katika Halmashauri hiyo hadi sasa
havijaingizwa kaika mfumo rasmi wa serikali na kumtaka
Mkurugenzi huyo kuviingiza ili kuepusha migogoro ambayo siyo ya lazima ambayo
inaweza kutokea.
“Mkurugenzi
nakuomba kila kiwanja unachopima katika Halmashauri yako hakikisha kuwa
kinaingizwa katika mfumo ili kuepusha migogoro ya ardhi
ambayo siyo ya lazima ambao inaweza kutokea baina ya serikali na wnanchi”,
Alisema Agelina
Pia Naibu Waziri
huyo aliwataka Wakurugenzi katika Wilaya ya Kahama kuhakikisha kuwa maeneo yote
ya umma yanapimwa ili kupunguza migogoro isiyokuwa na ulazima na kuongeza kuwa
iwapo halmashuari haitavipima viwanja vinaweza kuvamiwa na wananchi na mwisho
wa siku badala ya kupunguza migogoro tunakuwa tumeongeza tatizo.
COMMENTS