WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo...
WAZIRI wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na
kasi ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala Vigwaza Mkoani Pwani na
kumtaka mkandarasi Suma JKT kuongeza kasi na kuzingatia ubora.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akifafanua jambo wakati akikagua mchoro wa Bandari kavu ya Kwala –Vigwaza Mkoani Pwani. |
Akizungumza mara baada
ya kukagua ujenzi huo ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kushirikiana
na Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)
kuhakikisha wanaunganisha kwa haraka ili reli na barabara zinazoingia katika
bandari kavu hiyo zinakamilika na hivyo kuiwezesha bandari kavu hiyo kuanza
kutumika ifikapo Januari mwakani.
“TPA, TRL na TANROADS
uzuri wote mko kwenye wizara moja shirikianeni na hakikisheni kilomita 15 za
barabara inayoingia kwenye bandari kavu hii na kilomita moja ya reli zinajengwa
haraka,” Amesema Profesa Mbarawa.
Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa
maelekezo kwa Eng. Charles Salu Ogare anayesimamia ujenzi wa bandari kavu ya
Kwala-Vigwaza Mkoani Pwani.
|
Profesa Mbarawa amemtaka
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko kuhakikisha ujenzi wa bandari kavu
ya Kwala-Vigwaza unazingatia ubora na viwango vilivyopo katika mkataba ili
kuiwezesha kuhudumia zaidi ya makontena milioni moja kwa mwaka na hivyo
kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa mwenye kofia ya njano akiwa
katika majukumu ya ukaguzi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza
inayojengwa mkoani Pwani.
|
“Hakikisheni eneo la
bandari kavu linakuwa na maegesho ya kutosha, taa, maji ya uhakika, gari la
zimamoto, uzio na mashine ya ukaguzi wa mizigo scanner itakayowezesha kupima kila mzigo unaopandishwa na kushushwa
katika eneo hili,” amesisitiza Profesa Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
TPA Eng. Kakoko amesema TPA imejipanga kuhakikisha ujenzi huo unatumia gharama
nafuu na mifumo yote ya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA inakuwepo
katika bandari hiyo ili kuiwezesaha kufanya kazi kisasa na kwa ufanisi zaidi.
“Tukifanikiwa kuhamia
hapa mzigo uliokuwa unasafirishwa kwa siku saba sasa utatumia siku tatu kufika Mwanza
hali itakayovutia wasafirishaji wengi kutumia bandari ya Dar es Salaam na hivyo
kukuza uchumi wa nchi na kuibua fursa za ajira,” amesema Eng. Kakoko.
Muonekano wa bandari
kavu inayojengwa na mkandarasi Suma-KJT katika eneo la Kwala-Vigwaza
inayotarajiwa kuanza kutumika Januari mwakani ikiwa katika hatua mbalimbali za
ujenzi.
|
COMMENTS