Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ameshambuliwa na risasi karibu na nyumbani kwake jijini Dodoma akiwa nda...
Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ameshambuliwa na risasi karibu na nyumbani kwake jijini Dodoma akiwa ndani ya Gari.
Tundu Lissu |
Tukio hilo limetokea wakati Lissu akitoka nyumbani kwake na kuehudhuria kipindi cha mchana cha Bunge.
Repoti zinasema kuwa Lissu alishambuliwa na watu wasiofahamika ambao walimshambulia kwa risasi mfululizo akiwa ndani ya gari.
Kiongozi wa kambi pinzani Bungeni kupitia Chama cha upinzani CHADEMA Freeman Mbowe, alisema kuwa Lissu yupo katika hali mbaya.
“Juhudi za kuokoa maisha yake zinaendelea katika hospitali ya Mkoa Dodoma,” Mbowe alisema.
Hali ya kisiasa
Lissu amekuwa akikamatwa mara kwa mara ambapo katika kipindi kilichopita amekamatwa mara tisa na kushitakiwa mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa na maneno ya uchochezi ya kisiasa dhidi ya Rais John Magufuli na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Lissu, pia kwa sasa ni Rais wa Chama cha wanasheria Tanzania Law Society (TSL), amejitambulisha kama kiongozi wa upinzani Bungeni.
Pia Amekuwa akishutumu serikali mara kwa mara, akidai kuwa imeshindwa kukuza uchumi na kuboresha ustawi wa Watanzania.
COMMENTS