KUTOKANA na changamoto ya upungufu wa madarasa sanjari na walimu kufanyiakazi zao chini ya mti kwa kukosa ofisi katika shule ya msingi ...
KUTOKANA na changamoto
ya upungufu wa madarasa sanjari na walimu kufanyiakazi zao chini ya
mti kwa kukosa ofisi katika shule ya msingi Mhongolo wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga kumesababisha zaidi ya wanafuzi 200 kusomea
katika darasa moja.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mhongolo wakipata maelezo ya faida ya kunywa dawa hizo kutoka kwa Kaimu mganga mkuu Endrue Emmanuel hayupo pichani. |
Kutokana na hali
hiyo kumepelekea baadhi ya vikundi 30 vya wajasilia mali katika Kata hiyo
kuanza kuchangishana vitu mbalimbali vya vifaa vya ujenzi ikiwamo mifuko ya
saruji ili kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa mara moja ili kuwanusuru
wanafunzi.
Hayo yamesemwa
jana na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Helmani Ibengwe wakati wa
makabidhiano ya mifuko kumi ya saruji kati ya 30 iliyotolewa na baadhi ya
vikundi hivyo vya wajasilia mali kwa lengo la kusaidia ujenzi wa madarasa hayo
pamoja na ofisi ya walimu.
Ibengwe alisema
kuwa shule hiyo inaupungufu wa vyumba vya madarasa 33 huku mahitaji ni vyumba
46 na kuongeza kuwa kwa sasa vyumba vya madarasa vilivyopo ni 13 hali ambayo
inachangia mrundikano wa wanafunzi katika madarasa machache yaliyopo.
Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa shule hiyo yenye
jumla ya wanafunzi 2290 inahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali
yakiwamo mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali ili kuona umuhimu wa
kuisaidia shule hiyo ambayo imekuwa ikitegemea wajasiliamali wadogo wadogo wa
kilimo cha bustani na wafugaji wa kuku.
Mwenyekiti huyo
alisema kuwa pia mwaka jana vikundi hivyo vya wajasiliamali wa Kata hiyo kwa
kushirikiana na wananchi walifanikiwa kujenga vyumba viwili vya
madarasa na kuongeza kuwa watu wenye mapenzi mema wajitokeze kutoa
misaada yao.
Naye mwalimu
mkuu wa shule hiyo Leonida Daniel alisema kuwa naushukuru uongozi wa serikali
ya mtaa wa Mhongolo kwa kuvihamasisha vikundi kwani shule hiyo inaupungufu
mkubwa wa madarasa pamoja na changamoto ya walimu kufanyia kazi zao
chini ya mti badala ya kufanyia kazi hizo ofisini.
Pia mkuu huyo wa shule alisema kuwa changamoto nyingine iliyopo
ni upungufu wa vyoo vya wanafunzi kwani vilivyopo vinavyofanya kazi nane huku
16 bado havijakamilika na kuongeza kuwa mahitaji ya matundu ya vyoo katika
shule hiyo ni 91 na matundu yaliyopo ni 60 hivyo kulingana na idadi kubwa ya
wanafunzi 2290 haitoshi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Emmanuel Nangale alisema
kuwa kutokana na mrudikano mkubwa wa wanafunzi madarasani tayari
wameiandikia barua ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama
juu ya suala la kujenga shule nyingine na kuongeza kuwa maombi yao mkurugenzi
ayaharakishe ili ujenzi uanze mara moja.
Hata hivyo mjumbe wa serikali ya mtaa huo Mary Sumuni aliwataka
wadau wanaposikia watoto wanakosa mahitaji katika shule hiyo ni bora
wakajitokeza kusaidia badala ya kuwaacha wanafunzi wakiwa na mrundikano huo
uliopo sasa.
COMMENTS