Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatekeleza miradi miwili ya taa za kuongozea magari na abiria (traffic lights) jijini ...
Serikali
kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatekeleza miradi miwili ya taa za
kuongozea magari na abiria (traffic lights) jijini Tanga katika makutano ya
barabara za Taifa na Pangani
Akiongea
na Waandishi wa Habari Meneja wa Kikosi cha Umeme TEMESA Mhandisi Pongeza
Semakuwa alisema miradi hii miwili ya taa za barabarani hapo Tanga inahusisha taa
za kuongozea magari pamoja na zile za kuongoza waenda kwa miguu kuvuka makutano
hayo ya barabara. Taa hizo zitakuwa zikitumia umeme jua, nishati ambayo
itaziwezesha kufanya kazi muda wote hata pale umeme wa TANESCO unapokuwa na
hitilafu.
Nae
Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini Alhaj Mussa Mbaruku ambae alipita katika eneo la mradi la makutano
ya Barabara ya Pangani na Taifa maarufu kama “Taifa/Ring Junction” kujionea
utekelezaji huo wa mradi wa Serikali, alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo
kutapunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea kwenye makutano ya
barabara hizo na vile vile kuufanya mji wa Tanga kuwa wa kisasa zaidi.
Kwa
upande wake Meneja wa TEMESA Tanga Mhandisi Margareth Gina alisema kuwa miradi
hiyo ya usimikaji wa taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu jijini Tanga imeiingizia
TEMESA jumla ya shilingi za kitanzania milioni 434 fedha za Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania zitakazolipwa kwa TEMESA kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa
jiji la Tanga. Aliongeza kuwa miradi yote miwili iko mbioni kukamilika mapema
mwezi huu.
Mbunge wa Tanga Mjini Alhaj Mussa Mbaruku
akiongea na watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) alipofika katika
eneo la mradi wa kusimika taa za barabarani katika makutano ya barabara za
Taifa na Pangani jijini Tanga. Mradi huo wa kwanza kufanyika jijini Tanga
unahusiha taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu katika makutano ya
barabara za Taifa na pangazi pamoja na makutano ya barabara za Swahili, Uhuru
na ile ya Hospital ya Bombo. Taa hizo zitatumia nishati ya umeme jua. kutoka
kushoto ni Mhandisi Zuhura Semboja, Mhandisi Pongeza Semakuwa pamoja na
Mhandisi Margaret Gina.
COMMENTS