Habari Mpya

Habari Zote

Archive for 2017

Picha kutoka BBC SWAHILI



Uwanja wa michezo unaobeba watu 60,000 ulijaa huku raia wa Zimbabwe wakitaka kushuhudia kuapishwa kwa rais mpya.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUwanja wa michezo unaobeba watu 60,000 ulijaa huku raia wa Zimbabwe wakitaka kushuhudia kuapishwa kwa rais mpya.
Kuapishwa kwa bwana Mnangagwa kunafuatia kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe baada ya kuwa mamlakani kwa takriban miaka 37Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKuapishwa kwa bwana Mnangagwa kunafuatia kuondoka madarakani kwa Robert Mugabe baada ya kuwa mamlakani kwa takriban miaka 37
Bwana Mnangagwa alikuwa makamu wa rais wa Kwnaza ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu hatua iliosababisha jeshi kuingilia kati na kumshinikiza Mugabe kujiuzuluHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBwana Mnangagwa alikuwa makamu wa rais wa Kwnaza ambaye alifutwa kazi mapema mwezi huu hatua iliosababisha jeshi kuingilia kati na kumshinikiza Mugabe kujiuzulu
bwana Mnangagwa, ambaye alilitoroka taifa hilo alirudi kutoka mafichoni siku ya Jumatano tarehe 21 NovembaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionbwana Mnangagwa, ambaye alilitoroka taifa hilo alirudi kutoka mafichoni siku ya Jumatano tarehe 21 Novemba
Rais mpya na mkewe AxiliaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais mpya na mkewe Axilia
Bwana Mnangagwa amekuwa katikatiu ya urtawala wa Mugabe kwa takriban miaka 37Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBwana Mnangagwa amekuwa katikatiu ya urtawala wa Mugabe kwa takriban miaka 37
Mkuu wa jeshi jenerali Constantino Chiwenga, mtu aliyeongoza mapinduzi ya Robert Mugabe akitazama kuapishwa kwa MnangagwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMkuu wa jeshi jenerali Constantino Chiwenga, mtu aliyeongoza mapinduzi ya Robert Mugabe akitazama kuapishwa kwa Mnangagwa
Bwana Mnangagwa anashirikishwa na wengi na mabaya yaliofanyika chini ya utawala wa Zanu-PfHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBwana Mnangagwa anashirikishwa na wengi na mabaya yaliofanyika chini ya utawala wa Zanu-Pf
Katika hotuba yake alimsifu mtangulizi wake Robert MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKatika hotuba yake alimsifu mtangulizi wake Robert Mugabe
Pia aliahidi kuwatumia raia wote wa Zimbabwe , sio wanachama wa Zanu Pf pekee.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPia aliahidi kuwatumia raia wote wa Zimbabwe , sio wanachama wa Zanu Pf pekee.
Viongozi kutoka mataifa jirani ya Zimbabwe walihudhuriaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionViongozi kutoka mataifa jirani ya Zimbabwe walihudhuria
Alikuwa waziri wa zamani wa ulinzi , usalama na amekuwa na uhusiano wa karibu na JeshiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAlikuwa waziri wa zamani wa ulinzi , usalama na amekuwa na uhusiano wa karibu na Jeshi
Jeshi liliingilia kati na kumng'atua mamlakani Robert MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJeshi liliingilia kati na kumng'atua mamlakani Robert Mugabe
Umati mkubwa wa watu ulifurahia wakati wa kupigwa kwa mizingia 21 kama heshima ya kumkaribisha rais mpya huku ndege za kijesh zikiwa anganiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUmati mkubwa wa watu ulifurahia wakati wa kupigwa kwa mizingia 21 kama heshima ya kumkaribisha rais mpya huku ndege za kijesh zikiwa angani
Raia wengi wa Zimbabwe waliunga mkono hatua ya jeshi ya kuingilia kati kumuondoa MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRaia wengi wa Zimbabwe waliunga mkono hatua ya jeshi ya kuingilia kati kumuondoa Mugabe
UONGOZI wa hospitali ya misheni Kaibara, iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara, umetakiwa kubandika gharama za matibabu kwenye mbao za matangazo, ili kuondoa utata unaodaiwa kuwepo hospitalini hapo na kuleta manung’uniko kwa wananchi wanaokwenda kupata huduma ya matibabu katika hospitali hiyo.
Mkuu wa wilaya ya BundaLydia Bupilipili,

Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Bupilipili, wakati akizungumza na Radio Free Africa, kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo.

Bupilipili alisema kuwa amekuwa akipata malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi, wakidai kwamba gharama za matibabu katika hospitali hiyo ziko juu na kwamba zimekuwa hazieleweki vizuri kwa sababu haziwekwi kwenye mbao za matangazo.

Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa wilaya ya Bunda, aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kubandika kwenye mbao za matangazo gharama zote za matibabu ili kuondoa utata huo unaolalamikiwa na wananchi.

 “Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu hospitali ya Kibara, hasa kwenye gharama za matibabu. Sasa kupitia vyombo vya habari ninaagiza kuanzia sasa wawe wanabandika gharama za matangazo kwenye mbao za matangazo ili wananchi wazione” alisema.

Pia, alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikipatiwa ruzuku na serikali, ili iendelee kutoa huduma za matibabu kwa wananchi pasipo gharama, kwa makundi maalumu wakiwemo wazee wanaotambuliwa.


Halikadhalika mkuu huyo wa wilaya ya Bunda, aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutoa lugha zisizofaa kwa wauguzi na madaktari, kwani wanawavunja moyo wa kutekeleza wajibu wao, huku akiwataka wataalamu hao kuwajibika ipasavyo  ikiwa ni pamoja na kuacha vitendo vya kuomba rushwa.
SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limesema liko tayari kushirikiana na Serikali kujenga miundombinu ya kisasa ya usafiri, Nishati ya umeme, maji na usafi wa mazingira katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango(kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan(JICA), Hiroshi Kato walipokutana kwa mazungumzo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Hiroshi Kato wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Jijini Dar es Salaam.

Kato alisema kuwa mradi mwingine wanaotaka kuutekeleza katika mji wa Dodoma ni udhibiti wa taka ngumu na kwamba wanachosubiri ni Serikali kuainisha maeneo ya vipaumbele vilivyoko katika mpango mji wa Dodoma.

Aidha Makamu huyo wa Rais wa JICA alisema kuwa Shirika lake litaendelea kusaidia eneo la kilimo hususan kilimo cha mpunga ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuwakomboa wakulima.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amelishukuru Shirika hilo kwa kuonesha nia ya kusaidia ujenzi wa mji wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi.

Alisema kuwa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuupanga mji wa Dodoma mapema ili kuondoa changamoto za msongamano wa huduma za jamii kwenye eneo moja kama ilivyo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JICA nchini Tanzania Toshio Nagase, alioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Hiroshi Kato (katikati) walipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.


“Pamoja na umuhimu wa miundombinu ya maji, umeme, usafiri wa mjini, lakini pia tunataka tujenge mapema njia za juu (ring roads) ili kudhibiti msongamano wa magari” alisema Dk. Mpango.



Wajumbe walioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Hiroshi Kato wakifuatiia kwa makini majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato, Jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa mradi mwingine wa kipaumbele katika mji huo ni ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Msalato, karibu kilometa 20 kutoka katikati ya mji huo ili kurahisisha usafiri kwa njia ya anga.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazopata ufadhili mkubwa wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka Japan kupitia Shirika hilo la Kimataifa la Maendeleo (JICA).

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Isdor Mpango(kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Hiroshi Kato (hayupo pichani) katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa barabara ya juu (fly over) katika eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam, upanuzi wa awamu ya kwanza ya barabara mpya ya Bagamoyo (Mwenge-Tegeta) na ufadhili mpya wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Morocco hadi Mwenge.
Kamishina Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Shogholo Msangi akielezea kuhusu masuala ya kodi katika maendeleo ya Taifa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango na  Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Toshio Nagase, pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

SHIRIKA la utangazaji Nchini Zimbabwe (ZBC) limesema Makamu wa zamani wa rais wa nchini humo Emmerson Mnangagwa, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa.
Emmerson Mnangagwa

Mnangagwa, ambaye alitorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini humo ambapo kuondolewa kwake kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Mugabe.

Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane:
Katika barua yake Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu makabidhiano ya uongozi kwa njia ya amani na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.


Msemaji wa Zanu-PF alisema kuwa Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
TAFITI zinaeleza kuwa zipo baadhi ya dalili zinazojitokeza katika mwili wa binadamu ambazo katika hali isiyo ya kawaida ni ishara kuwa mwili huo una shida na unahitaji uchunguzi kugundua ni tatizo la aina gani. 

Baadhi ya dalili hizo zilizoelezwa na tafiti hasa kwa watoto wadogo zinazoashiria kupatwa na ugonjwa wa saratani ni kuvimba sehemu ya mwili bila maumivu yoyote  hasa sehemu za  shingo, miguu, shavu na tumboni.

Akizungumza na Raia Tanzania mapema wiki hii, Katibu wa Shirikisho la Vyama  vya Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala (SHIVYATIATA),  lenye makao yake Tabaa Relini Jijini Dar es Salaam Dk. Othuman Shem alisema baadhi ya dalili katika mwili wa binadamu  ni ishara ya ugonjwa wa saratani ingawa kundi kubwa la watu halina ufahamu huo.

Dk. Shem ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha dawa za asili cha  Paseko Natural Clinic  alisema  utafiti uliofanywa na kampuni ya Paseko T.O & P. Co. Ltd  kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ireland  hapa nchini,  ulionesha kuwapo kwa kundi kubwa la watu katika hamii hasa watoto kuwa na dalili hizo bila kujua kuwa ni dalili za saratani hasa watoto.
Image result for picha ya mtoto mwenye uvimbe wa saratani
Picha ya mtoto mwenye uvimbe.

 “Katika hatua ya kuangalia dalili hizo kwa kushirikiana na ubalozi wa Ireland hapa nchini, tumegundua kuwa zaidi ya asilimia 67 ya dalili hizi inaonesha kuwa huu ni ugonjwa wa saratani lakini wengi  hawajui.”alisema Dk. Shem.

Aliendelea kusema kuwa dalili zingine ni pamoja na mtoto  wa jicho kuwa na rangi nyekundu, makengeza na hata upofu wa ghafla.

“Pia damu kutoka kwenye fizi, kuvia katika macho, kutapika wakati wa asubuhi, kuumwa na  kichwa kupitiliza, kukonda bila sababu, kupungua uzito, homa inayojirudia rudia bila kuwa na chanzo, nguvu ya mwili kupungua kuliko kawaida” alisema. Othuman.

Zaidi ya dalili hizo, nyingine ni  mtoto  kupungua damu mwilini mara kwa mara, alisema na kuongeza: “Tunaendelea kufanya tafiti zaidi ili kuweza kuokoa  Watanzania, hii ni pamoja na kutoa elimu hasa vijijini ambako wengi wanakuwa na dalili hizi lakini hawazijui na kujikuta wakipoteza maisha ama watoto au wapendwa wao,”aliongeza.

Kwa muktadha huo, alisema kampuni  hiyo  imeamua kujitolea  kwa kushirikiana na mamlaka zingine kupima bure watoto wenye  dalili hizo nchini kote na kusema kuwa milango iko wazi kwa Mtanzania mwenye hitaji 
SPIKA wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters limemnukuu Jacob Mudenda hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake huku Spika wa bunge akisema kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.

Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.
Mugabe ambaye ameingia madarakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980 alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka madalakani wiki hii.

Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake huku sababu za kumtaka ang’atuke zikiwa ni baada ya kumfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.

Hatua hiyo ilionekana na wengi kama njama ya kumrithisha mkewe na kusababisha viongozi wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizini.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala wa kiongozi huyo.

Amesema kuwa Uingereza ambaye ni rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.

Ubalozi wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao kwakile kilichodaiwa kuwa ni wakati wa mabadiliko.

Kwa mujibu wa Mwanaharakati wa haki za Binadamu Linda Masarira akiongea na BBC ninafuraha sana leo kwa sababu nimekuwa nikiamini kwamba Mugabe atajiuzulu katika maisha yangu.

Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kilifurahia hatua hiyo kikisema kuwa Mugabe alibadilika kutoka kuwa mkombozi hadi dikteta.

''Na sasa kwenda mbele ni wakati wa upinzani kujiandaa na kuona kwamba tunakuwa na serikali inayowajali raia wake.Na kila mtu lazima ashirikishwe''.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kufanya kazi kwa bidii katika miradi yote inayopewa na Serikali ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa (katikati), akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga (kulia) wakati akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.


Akikagua hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni kota, Kwandikwa, amesema Serikali itaendelea kuainisha miradi mingine ili kuhakikisha fedha za Serikali zinaokolewa na kusimamiwa kwa uzalendo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa (katikati), kuhusu hatua zilizofikiwa katika utelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi huo, jijini Dar es Salaam.

“Hakikisheni mnafanya kazi zenu kwa weledi, uzalendo na kukamilisha miradi kwa wakati na kuokoa fedha ambazo zitatumika katika utekelezaji wa miradi mingine hapa nchini”, amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Muonekano wa mtambo wa kuchakata zege unaotumiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam.

Ametoa wito kwa wataalamu wengine kuja kupata mafunzo kwa TBA ambao ni chachu ya utekelezaji wa miradi mingi hapa nchini kwa kuwa wanatumia mfumo wa kisayansi na mitambo yenye kusaidia kupunguza gharama za ujenzi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam.

Pia, Naibu Waziri huyo ameushukuru uongozi wa TBA kwa kutoa ajira za vibarua takribani 200 kwa siku katika mradi huo na kuwataka  wafanyakazi hao kuwa waadilifu na waaminifu ili kuwa na sifa za kupata ajira za kudumu.
Muonekano wa baadhi ya vitalu vya makazi eneo la Magomeni Kota zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 35.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kukamilika mradi huo kwa wakati, ubora na kwa gharama nafuu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Elias Kwandikwa, akizungumza na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati alipowatembelea wakala huo leo, jijini Dar es Salaam.

Amefafanua kuwa mradi huo utakuwa una jumla ya vitalu vitano ambapo vitalu vinne vina majengo ya ghorofa nane na kitalu kimoja kina jengo la ghorofa tisa na hivyo mradi utatoa makazi kwa kaya 656.
Meneja Rasilimali Watu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Gerwalda Luoga, akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (hayupo pichani) mara baada ya kikao kazi na Naibu Waziri huyo, jijini Dar es Salaam.

Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi mwakani na utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 20 zote ikiwa ni fedha za Serikali.

- Copyright © Mito Ya Baraka Morogoro - Mito Ya Baraka Morogoro - Powered by Blogger - Designed by Peter Mwamkamba -