Picha kutoka BBC SWAHILI
Habari Zote
Archive for November 2017















UONGOZI wa hospitali ya
misheni Kaibara, iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara, umetakiwa kubandika
gharama za matibabu kwenye mbao za matangazo, ili kuondoa utata unaodaiwa
kuwepo hospitalini hapo na kuleta manung’uniko kwa wananchi wanaokwenda kupata
huduma ya matibabu katika hospitali hiyo.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya BundaLydia Bupilipili, |
Kauli hiyo ilitolewa
jana na mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Bupilipili, wakati akizungumza na Radio
Free Africa, kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu huduma
zinazotolewa katika hospitali hiyo.
Bupilipili alisema kuwa
amekuwa akipata malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi, wakidai
kwamba gharama za matibabu katika hospitali hiyo ziko juu na kwamba zimekuwa
hazieleweki vizuri kwa sababu haziwekwi kwenye mbao za matangazo.
Kufuatia malalamiko
hayo mkuu wa wilaya ya Bunda, aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kubandika
kwenye mbao za matangazo gharama zote za matibabu ili kuondoa utata huo
unaolalamikiwa na wananchi.
“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka
kwa wananchi kuhusu hospitali ya Kibara, hasa kwenye gharama za matibabu. Sasa
kupitia vyombo vya habari ninaagiza kuanzia sasa wawe wanabandika gharama za
matangazo kwenye mbao za matangazo ili wananchi wazione” alisema.
Pia, alisema kuwa
hospitali hiyo imekuwa ikipatiwa ruzuku na serikali, ili iendelee kutoa huduma
za matibabu kwa wananchi pasipo gharama, kwa makundi maalumu wakiwemo wazee
wanaotambuliwa.
Halikadhalika mkuu huyo
wa wilaya ya Bunda, aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutoa lugha zisizofaa
kwa wauguzi na madaktari, kwani wanawavunja moyo wa kutekeleza wajibu wao, huku
akiwataka wataalamu hao kuwajibika ipasavyo
ikiwa ni pamoja na kuacha vitendo vya kuomba rushwa.
SHIRIKA
la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limesema liko tayari kushirikiana na
Serikali kujenga miundombinu ya kisasa ya usafiri, Nishati ya umeme, maji na
usafi wa mazingira katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma.
Ahadi
hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Hiroshi Kato wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip
Mpango, Jijini Dar es Salaam.
Kato alisema kuwa mradi mwingine wanaotaka kuutekeleza katika mji wa Dodoma ni
udhibiti wa taka ngumu na kwamba wanachosubiri ni Serikali kuainisha maeneo ya
vipaumbele vilivyoko katika mpango mji wa Dodoma.
Aidha
Makamu huyo wa Rais wa JICA alisema kuwa Shirika lake litaendelea kusaidia eneo
la kilimo hususan kilimo cha mpunga ili kuongeza thamani ya zao hilo na
kuwakomboa wakulima.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amelishukuru Shirika hilo kwa kuonesha
nia ya kusaidia ujenzi wa mji wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi.
Alisema
kuwa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuupanga mji wa Dodoma mapema ili
kuondoa changamoto za msongamano wa huduma za jamii kwenye eneo moja kama
ilivyo Jijini Dar es Salaam.
“Pamoja
na umuhimu wa miundombinu ya maji, umeme, usafiri wa mjini, lakini pia tunataka
tujenge mapema njia za juu (ring roads) ili kudhibiti msongamano wa magari”
alisema Dk. Mpango.
Aliongeza
kuwa mradi mwingine wa kipaumbele katika mji huo ni ujenzi wa uwanja wa ndege
wa kimataifa katika eneo la Msalato, karibu kilometa 20 kutoka katikati ya mji
huo ili kurahisisha usafiri kwa njia ya anga.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazopata ufadhili mkubwa wa miradi mbalimbali
ya maendeleo kutoka Japan kupitia Shirika hilo la Kimataifa la Maendeleo (JICA).
Baadhi
ya miradi hiyo ni ujenzi wa barabara ya juu (fly over) katika eneo la Tazara
Jijini Dar es Salaam, upanuzi wa awamu ya kwanza ya barabara mpya ya Bagamoyo (Mwenge-Tegeta)
na ufadhili mpya wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hiyo kutoka Morocco
hadi Mwenge.
Mazungumzo
hayo yamehudhuriwa pia na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa
la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Toshio Nagase, pamoja na
Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA.
SHIRIKA
la utangazaji Nchini Zimbabwe (ZBC) limesema Makamu wa zamani wa rais wa nchini
humo Emmerson Mnangagwa, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa
kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa.
![]() |
Emmerson Mnangagwa |
Mnangagwa,
ambaye alitorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo
Jumatano nchini humo ambapo kuondolewa kwake kwake madarakani kulisababisha
chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala
wa miaka 37 wa Mugabe.
Taarifa
hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane:
Katika
barua yake Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu makabidhiano ya
uongozi kwa njia ya amani na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.
Msemaji
wa Zanu-PF alisema kuwa Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika
kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
TAFITI zinaeleza kuwa zipo baadhi ya dalili zinazojitokeza katika mwili wa binadamu ambazo katika hali isiyo ya kawaida ni ishara kuwa mwili huo una shida na unahitaji uchunguzi kugundua ni tatizo la aina gani.
Baadhi ya dalili hizo zilizoelezwa na tafiti hasa kwa watoto wadogo zinazoashiria kupatwa na ugonjwa wa saratani ni kuvimba sehemu ya mwili bila maumivu yoyote hasa sehemu za shingo, miguu, shavu na tumboni.
Akizungumza na Raia Tanzania mapema wiki hii, Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala (SHIVYATIATA), lenye makao yake Tabaa Relini Jijini Dar es Salaam Dk. Othuman Shem alisema baadhi ya dalili katika mwili wa binadamu ni ishara ya ugonjwa wa saratani ingawa kundi kubwa la watu halina ufahamu huo.
Dk. Shem ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha dawa za asili cha Paseko Natural Clinic alisema utafiti uliofanywa na kampuni ya Paseko T.O & P. Co. Ltd kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ireland hapa nchini, ulionesha kuwapo kwa kundi kubwa la watu katika hamii hasa watoto kuwa na dalili hizo bila kujua kuwa ni dalili za saratani hasa watoto.
Picha ya mtoto mwenye uvimbe. |
“Katika hatua ya kuangalia dalili hizo kwa kushirikiana na ubalozi wa Ireland hapa nchini, tumegundua kuwa zaidi ya asilimia 67 ya dalili hizi inaonesha kuwa huu ni ugonjwa wa saratani lakini wengi hawajui.”alisema Dk. Shem.
Aliendelea kusema kuwa dalili zingine ni pamoja na mtoto wa jicho kuwa na rangi nyekundu, makengeza na hata upofu wa ghafla.
“Pia damu kutoka kwenye fizi, kuvia katika macho, kutapika wakati wa asubuhi, kuumwa na kichwa kupitiliza, kukonda bila sababu, kupungua uzito, homa inayojirudia rudia bila kuwa na chanzo, nguvu ya mwili kupungua kuliko kawaida” alisema. Othuman.
Zaidi ya dalili hizo, nyingine ni mtoto kupungua damu mwilini mara kwa mara, alisema na kuongeza: “Tunaendelea kufanya tafiti zaidi ili kuweza kuokoa Watanzania, hii ni pamoja na kutoa elimu hasa vijijini ambako wengi wanakuwa na dalili hizi lakini hawazijui na kujikuta wakipoteza maisha ama watoto au wapendwa wao,”aliongeza.
SPIKA wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters limemnukuu Jacob Mudenda hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake huku Spika wa bunge akisema kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya Jumatano.
Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.
Mugabe ambaye ameingia madarakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980 alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka madalakani wiki hii.
Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake huku sababu za kumtaka ang’atuke zikiwa ni baada ya kumfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.
Hatua hiyo ilionekana na wengi kama njama ya kumrithisha mkewe na kusababisha viongozi wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizini.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala wa kiongozi huyo.
Amesema kuwa Uingereza ambaye ni rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.
Ubalozi wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao kwakile kilichodaiwa kuwa ni wakati wa mabadiliko.
Kwa mujibu wa Mwanaharakati wa haki za Binadamu Linda Masarira akiongea na BBC ninafuraha sana leo kwa sababu nimekuwa nikiamini kwamba Mugabe atajiuzulu katika maisha yangu.
Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kilifurahia hatua hiyo kikisema kuwa Mugabe alibadilika kutoka kuwa mkombozi hadi dikteta.
''Na sasa kwenda mbele ni wakati wa upinzani kujiandaa na kuona kwamba tunakuwa na serikali inayowajali raia wake.Na kila mtu lazima ashirikishwe''.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kufanya kazi kwa bidii katika miradi yote inayopewa na Serikali ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Akikagua hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni kota, Kwandikwa, amesema Serikali itaendelea kuainisha miradi mingine ili kuhakikisha fedha za Serikali zinaokolewa na kusimamiwa kwa uzalendo.
“Hakikisheni mnafanya kazi zenu kwa weledi, uzalendo na kukamilisha miradi kwa wakati na kuokoa fedha ambazo zitatumika katika utekelezaji wa miradi mingine hapa nchini”, amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Muonekano wa mtambo wa kuchakata zege unaotumiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota, jijini Dar es Salaam. |
Ametoa wito kwa wataalamu wengine kuja kupata mafunzo kwa TBA ambao ni chachu ya utekelezaji wa miradi mingi hapa nchini kwa kuwa wanatumia mfumo wa kisayansi na mitambo yenye kusaidia kupunguza gharama za ujenzi.
Pia, Naibu Waziri huyo ameushukuru uongozi wa TBA kwa kutoa ajira za vibarua takribani 200 kwa siku katika mradi huo na kuwataka wafanyakazi hao kuwa waadilifu na waaminifu ili kuwa na sifa za kupata ajira za kudumu.
Muonekano wa baadhi ya vitalu vya makazi eneo la Magomeni Kota zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 35.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kukamilika mradi huo kwa wakati, ubora na kwa gharama nafuu.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kukamilika mradi huo kwa wakati, ubora na kwa gharama nafuu.
Amefafanua kuwa mradi huo utakuwa una jumla ya vitalu vitano ambapo vitalu vinne vina majengo ya ghorofa nane na kitalu kimoja kina jengo la ghorofa tisa na hivyo mradi utatoa makazi kwa kaya 656.
Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi mwakani na utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 20 zote ikiwa ni fedha za Serikali.